LIVE STREAM ADS

Header Ads

TANZANIA IKO TAYARI KWA MCHEZO WA KWANZA AFCON 2025

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Tanzania inaanza kampeni yake ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) leo kwa mtihani mzito dhidi ya vigogo Nigeria, kabla ya kuwakabili Uganda siku nne baadaye na kisha kumaliza hatua ya makundi dhidi ya Tunisia tarehe 30 Desemba.

Nigeria na Tanzania zitakutana katika AFCON kwa mara ya pili. Mechi pekee waliyokutana awali kwenye fainali hizi ulikuwa mwaka 1980, wakati Nigeria walipoifunga Tanzania 3-1 katika mechi ya ufunguzi huko Lagos, kabla ya kutwaa ubingwa wao wa kwanza wa Afrika.

Kwa ujumla, timu hizo zimekutana mara nane katika mashindano yote. Nigeria hawajawahi kufungwa na Tanzania, wakishinda mechi tano na kutoka sare tatu.

Michezo yao waliyokutana hivi karibuni ilikuwa katika kufuzu AFCON 2017, walitoka sare ya 0-0 Dar es Salaam kabla ya Nigeria kushinda 1-0 mjini Uyo.

Chini ya kocha Miguel Gamondi, Taifa Stars wamewasili kwenye fainali hizi wakiwa na mchanganyiko wa wachezaji wanaocheza nje ya nchi na nyota wa ndani kutoka klabu kubwa za Tanzania Simba SC, Yanga na Azam FC.

Huu ni ushiriki wa nne wa Tanzania katika AFCON, ikiwa ni mara ya pili mfululizo kufuzu.

Tanzania wamepangwa Kundi A linalotajwa kuwa moja ya magumu zaidi, likiwajumuisha Nigeria, Tunisia na majirani Uganda. 

No comments:

Powered by Blogger.