LIVE STREAM ADS

Header Ads

SIMA ACHAGULIWA TENA MEYA JIJI LA MWANZA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com 
Diwani wa Kata ya Mhandu kupitia Chama Cha mapinduzi (CCM), Constantine Sima amechaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Mwanza kwa mara ya pili baada ya kupata kura zote 26 zilizopigwa na wajumbe wa baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo.

Uchaguzi huo umefanyika leo Jumanne Disemba 02, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Sima amesema atashirikiana vyema na madiwani pamoja na wananchi katika kuhakikisha maendeleo yanapatika.

"Wananchi wametuamini, wakatuchagua ili tuwatumike hivyo nitashirikiana na madiwani wenzangu ili tuweze kufanya kazi nzuri itakazoleta tija kwenye jamii" amesema  Sima.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sima Costantine.

No comments:

Powered by Blogger.