LIVE STREAM ADS

Header Ads

Madiwani Mwanza watakiwa kuwainua vijana kiuchumi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wametakiwa kutumia fursa za kimaendeleo zilizopo katika maeneo yao kwaajili ya kuwainua vijana kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa Jumanne Disemba 02, 2025 na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, John Nzilanyingi wakati akizungumza kwenye baraza la kwanza la madiwani.

Amesema mwanza kuna ziwa Victoria ambalo wakilitumia vizuri linaweza kuchochea ukuaji wa uchumi hususani kwa vijana.

"Tukitengeneza moango mkakati wa kuwakusanya vijana ambao wako tayari kujihusisha na shughuli za uvuvi tukawapeleka kwenye chuo cha uvuvi Nyegezi ili wapate elimu ya kutosha, watakapohitimu tuwape mikopo kwaajili ya kuanza rasmi shughuli za ufugaji wasamaki kwa njia ya vizimba na jamii itanufaika na ziwa hilo kwakupata kitoweo na fedha" amesema Nzilanyingi.

Amesema vijana ndio taa ya nchi hivyo wanapaswa kuwekeza nguvu kubwa kwenye kuwanyanyua ili waweze kujikwamua kiuchumi hatua itakayosaidia kupunguza changamoto ya ajira kwa kundi hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana, Peter Bega amewaasa madiwani kufanya kazi kwakufuata maadili.

"Mnapoona kuna mianya ya rushwa semeni na mkemee vikali kwaajili ya kulinda fedha zinazoletwa kutekeleza miradi mbalimbali katika maeneo yenu kwani mkifanya hivyo mtasaidia miradi mingi kutekelezwa kwa viwango vya juu na kukamilika kwa wakati" amesema Bega.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi amewakumbusha madiwani kuwa wananchi wanasubiri ahadi walizoziahidi hivyo wakafanye kazi ya kuwahudumia wananchi ikiwemo kuwaletea maendeleo.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Costantine Sima.
Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Anitha Rwezaula.

No comments:

Powered by Blogger.