LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIJANA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO TADB

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Vijana mkoani Mwanza wamehimizwa kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa bila riba na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), ili kuanzisha na kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kilimo, uvuvi na ufugaji.

Rai hiyo imetolewa Jumatano Disemba 03, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari na wahariri wa vyombo vya habari mkoani Mwanza, yaliyoandaliwa na Benki ya TADB.

Mtanda amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2024/25 jumla ya shilingi bilioni 7.5 zimetolewa kwa vijana kama mkopo usio na bila riba na na benki ya TADB kwa vijana 350 wanaofanya shughuli za uvuvi wa kisasa wa kutumia vizimba walio katika vikundi 47 ambapo tayari vijana hao wameanza kupata faida na kurejesha shilingi bilioni 1.3 kwa awamu ya kwanza.

Katika hatua nyingine Mtanda amewahamasisha wanahabari mkoani Mwanza pia kuchangamkia fursa hiyo kwa na kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kupitia mikopo hiyo nao waweze kujikwamua kiuchumi.

Awali akizungumza kwenye mafunzo hayo, Meneja wa TADB Kanda ya Ziwa, Alphonce Mokoki amesema lengo kubwa la benki hiyo iliyoanzishwa na Serikali mwaka 2015 ni kuwawezesha wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi huku pia nchi ikijiimarisha katika katika upatikanaji wa chakula.

Mokoki amebainisha kuwa benki ya TADB tayari imetoa kiasi cha shulingi bilioni 79.14 kama mkopo kwa vijana ambayo wameingia katika mnyoyoyo wa kuongeza thamani mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi.

Kwa upande wake Michael Obunde ambaye ni mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo amesema vijana wengi wanakosa taarifa sahihi kuhusu fursa zilizopo ikiwemo mikopo hivyo mafunzo hayo yatasaidia wanahabari kufikisha uelewa kwa jamii.

"Ni vizuri wananchi hasa vijana wakatambua ni wapi pa kupata taarifa sahihi, tunao wajibu wa kuwaelimisha kwamba badala ya kujinda kwenye mitandao ya kijamii wakifuatilia taarifa zisizo na tija, ni vyema wakafuatilia kurasa kama za benki ya TADB ili wasipitwe na fursa zilizopo" amesema mwanahabari Hellen Mtereko.
Na George Binagi, BMG
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda.
Meneja wa TADB Kanda ya Ziwa, Alphonce Mokoki.
Wanahabari mkoani Mwanza.
Wanahabari.
Wanahabari.
Wanahabari wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda na watumishi wa TADB.
Wanahabari wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda na watumishi wa TADB.

No comments:

Powered by Blogger.