LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAJUMBE KUTOKA NORWAY WATEMBELEA SHIRIKA LA KIVULINI JIJINI MWANZA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la kutetea haki za wanawake la KIVULINI lenye ofisi zake kuu Nyamhongolo jijini Mwanza, Jumatatu Februari 09, 2026 limepokea ugeni kutoka nchini Norway wenye lengo la kushuhudia utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na shirika hilo.

Ugeni huo umejumuisha Wajumbe wa Kamati Tendaji kutoka shirika la FO Innlandet, FOKUS na Mwakilishi wa Balozi wa Norway nchini Tanzania ambapo mashirika hayo ni miongoni mwa wafadhili wa miradi ya kutokomeza ukatili wa kijinsia inayotekelezwa na shirika la KIVULINI.

Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally amesema ziara ya wajumbe hao katika shirika hilo itadumu kwa muda wa siku tatu kuanzia Jumatatu Februari 09, 2026 hadi  Jumatano Februari 11, 2026 ambapo watapata fursa ya kukutana na viongozi, wadau na wananchi waliojengewa uwezo na KIVULINI ili kusaidia kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji na mimba za utotoni.

"Kupitia ugeni huu, tunategemea kuimaimarisha zaidi ushirikiano na ubalozi wa Norway, wafadhili wetu shirika la FOKUS na FO na hivyo kufikisha elimu ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wananchi wengi" amesema Ally.

Naye Kiongozi wa ujumbe huo, Ole Henrik Krakenes kutoka shirika la FO, amesema wanatarajia kuona na kujifunza mbinu mbalimbali ikiwemo ya SASA zinazotumiwa na shirika la KIVULINI kufikisha elimu kwa jamii ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake, ukeketaji na ndoa za utotoni.

Krakenes amesema Norway ina furaha kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo ya kutokomeza ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha wanawake wanakuwa salama katika jamii, akisema wamekuwa wakiona kazi nzuri inayofanywa na shirika la KIVULINI hivyo ziara yao inalenga kujionea kwa vitendo mafanikio yaliyofikiwa kupitia miradi inayofadhiliwa na shirika la FO kupitia shirika la FOKUS.
Na George Binagi, Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha taarifa ya shughuli zinazofanywa na shirika hilo katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza,  Mara, Shinyanga na Kigoma katika kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akionyesha jedwali lenye takwimu za ukatili wa kijinsia baada ya kupungua ikiwa ni jitihada za shirika hilo kwa kushirikiana na wadau pamoja na Serikali.
Timu ya viongozi na wawakilishi kutoka nchini Norway wakifuatilia taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally kuhusu shughuli zinazotekelezwa na shirika hilo. Shirika la FOKUS kutoka Norway linafadhili mradi wa kutokomeza ukeketaji na ndoa za utotoni unaotekelezwa na shirika la KIVULINI.
Afisa Miradi Mwandamizi Shirika la KIVULINI, Grace Mussa akitoa taarifa ya utekelezaji miradi ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa timu ya wafadhili kutoka shirika la FOKUS na FO kutoka Norway.
Afisa Miradi Mwandamizi Shirika la KIVULINI, Eunice Mayengelea akieleza utekelezaji wa miradi ya kuzuia ukatili wa kijinsia inayotekelezwa na shirika hilo.
Mjumbe wa Kamati Tendaji kutoka Shirika la FO la nchini Norway, Ole Henrik Krakenes (aliyesimama) akizungumza jambo walipotembelea ofisi za shirika la KIVULINI jijini Mwanza.
Mjumbe wa Kamati Tendaji Shirika la FO Innlandet, David Forsell akifafanua jambo baada ya kutembelea ofisi za shirika la KIVULINI.
Mwakilishi wa Balozi wa Norway nchini Tanzania, Anette Pettersen (kushoto) akiwa na wajumbe wa Kamati Tendaji shirika la FO kutoka Norway wakati wa ziara yao katika ofisi za shirika la KIVULINI jijini Mwanza.
Wawakili kutoka mashirika la FO na FOKUS ya nchini Norway wakiwa katika ofisi ya shirika la KIVULINI jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia) akizungumza na ujumbe kutoka nchini Norway uliotembelea ofisi za shirika hilo zilizopo Nyamhongolo jijini Mwanza.
Wageni hao wamelakiwa na burudani ya ngoma ya kabila la wasukuma.
Wajumbe kutoka shirika la FO, FOKUS na Mwakilishi wa Balozi wa Norway nchini Tanzania wakiwa katika ofisi za shirika la KIVULINI jijini Mwanza.
Burudani ya ngoma ya kabila la wasukuma.
Wajumbe wa Kamati Tendaji kutoka shirika la FO wakifuatilia ripoti ya utekelezaji wa mradi ya kutokomeza ukatili wa kijinsia inayotekelezwa na shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la FOKUS kupitia FO kutoka nchini Norway.

No comments:

Powered by Blogger.