LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIRIKA LA KIVULINI LASAIDIA UKATILI WA KIJINSIA KUPUNGUA MWANZA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Imeelezwa kuwa jitihada zinazofanywa na shirika la kutetea haki za wanawake la KIVULINI kwa kushirikiana na Serikali pamoja na Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia la Wanawake na Watoto zimesaidia kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia mkoani Mwanza.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP. Wilbroard Mutafungwa kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nyamagana, SP. Virginia Sodoka wakati shirika la KIVULINI na wafadhili wake kutoka nchini Norway walipotembelea ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto Nyamagana.

Amesema jitihada hizo ambazo ni pamoja na kuwajengea uwezo viongozi wa dawati la jinsia na watoto, maaskari wapelelezi na elimu kwa jamii zimesaidia matukio ya ukatili wa kijinsia kufichuliwa na kushughulikiwa kwa wakati hatua ambayo imesaidia kushuka hadi asilimia 23 kwa ngazi ya Mkoa wa Mwanza.

Naye Mkuu wa Dawati la Polisi la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mwanza, Faraja Mkinga amesema jamii imekuwa na mwamko wa kufichua matukio ya ukatili wa kijinsia kutokana na elimu inayotolewa na wadau ikiwemo Shirika la KIVULINI hatua ambayo imesaidia kupambana na matukio hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally amesema tangu mwaka 2014 limekuwa likitekeleza mradi wa kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia mkoani Mwanza kwa ufadhili wa shirika la FOKUS kutoka nchini Norway ambapo wamejenga uwezo kwa makundi mbalimbali ikiwemo klabu za wanafunzi, vikundi vya wanawake, madawati ya polisi na wanaharakati wa kujitolea hatua ambayo imesaidia kufikisha elimu katika jamii.

Naye Kiongozi wa ujumbe huo, Ole Henrik Krakenes kutoka shirika la FO la nchini Norway ameeleza kuvutiwa na muundo wa dawati la polisi la jinsia na watoto Nyamagana mkoani Mwanza hasa chumba maalumu cha usiri kwa ajili ya kushughulikia mashauri ya ukatili wa kijinsia hivyo wamekuwa na wakati mzuri wa kujifunza.
Na George Binagi, Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akieleza namna Shirika hilo linavyoshirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto kushughulikia mashauri ya ukatili wa kijinsia.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Nyamagana, SP. Virginia Sodoka akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza wakati wafadhili kutoka Norway walipotembelea Dawati la Jinsia na Watoto Nyamagana mkoani Mwanza.
Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mwanza, Faraja Mkinga.
Mjumbe wa Kamati Tendaji kutoka Shirika la FO la nchini Norway, Ole Krakenes akizungumza kuhusu ujio wao jijini Mwanza kujifunza jitihada zinazofanyika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mjumbe wa Kamati Tendaji kutoka Shirika la FO la nchini Norway, Ole Krakenes akizungumza kuhusu ujio wao jijini Mwanza kujifunza jitihada zinazofanyika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mwakilishi wa Balozi wa Norway nchini Tanzania, Anette Pettersen akitoa salamu zake wakati ujumbe kutoka mashirika ya FO na FOKUS ya nchini Norway ulipotembelea Dawati la Jinsia na Watoto Nyamagana mkoani Mwanza. Norway imekuwa ikifadhili utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na shirika la KIVULINI.
Askari mkoani Mwanza wakimsikiliza Mwakilishi wa Balozi wa Norway nchini Tanzania, Anette Pettersen
Mkurugenzi wa Mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kutoka Shirika la FOKUS la nchini Norway, Mildrid Mikkelsen akitoa salamu. Shirika la FOKUS linafadhili mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na shirika la KIVULINI la nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kutoka Shirika la FOKUS la nchini Norway, Mildrid Mikkelsen akitoa salamu.
Mjumbe wa Kamati Tendaji Shirika la FO Innlandet, David Forsell akieleza matarajio ya kufika jijini Mwanza ili kujifunza mbinu za kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Wawakilishi kutoka Norway wakipata maelekezo jinsia Dawati la Polisi la Jinsia la Watoto Nyamagana mkoani Mwanza linavyofanya kazi.
Tazama Video hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.