WAFANYABIASHARA MWANZA WAONYWA UTUPAJI TAKA KWENYE MITARO
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Baraza la Wafanyabiashara ngazi ya Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, limewataka wafanyabiashara kuacha tabia utupaji wa taka ovyo katika mitaro hatua itakayosaidia kuepuka athari mbalimbali ikiwemo uharibifu wa barabara.
Wajumbe wa baraza hilo waliyasema hayo Jumanne Feburuari 11, 2026 walipokuwa kwenye kikao chao kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Akizungumza kwa niaba ya Meneja wa TARURA Wilaya ya Nyamagana, Mhandisi Christopher Mwigamba alisema Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwaajili ya matengenezo na ujenzi wa Barbara katika maeneo mbaimbali kwa kiwango Cha rami,zege na changarawe.
Alisema pamoja na kupokea fedha hizo na kuzisimamia vizuri kwaajili ya utekekezaji wa ujenzi wa Barbara bado wanakumbana na changamoto ya mitaro kuziba hususani katika maeneo ya katikati ya mji inayosababishwa na wafanyabiashara kutupa takataka.
"Mitaro inapoziba inasababisha barabara kuharibika kwa haraka zaidi hivyo ni vyema wafanyabiashara wakaacha kutupa takataka ili barabara ziweze kutuhudumia kwa muda mrefu" aliseama Mhandisi Mwigamba.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wavuvi Mkoa wa Mwanza, Bakari Kadabi alisema wafanyabiashara wanapotupa taka kwenye mitaro zinasafiri moja kwa moja hadi ziwani na zinakwenda kuharibu mazalia ya samaki na hivyo kusababisha samaki kupungua ziwani.
Naye Mwenyekiti wa Soko Kuu la Mwanza, Hamad Nchola aliwaomba wajumbe wa baraza hilo kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha changamoto ya utupaji wa takataka kwenye mitalo inaondolewa Kwa haraka.
Akizungumzia suala hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Thomas Salala aliwasihi wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwakufuata sheri,kanuni na taratibu za nchi.
"Mnaotupa takataka kwenye mitaro mnakuwa mnavunja sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa hivyo mnatakiwa kuzingatia suala la usafi wa mazingira kwa kuacha tabia ya kutupa takataka ovyo hususani kwenye mitaro" alisema Salala.



No comments: