LIVE STREAM ADS

Header Ads

SEHEMU YA PILI: TARIME ZIPO MILA ZA KUKUMBATIA, LAKINI SI UKEKETAJI.


Wasichana Wakikeketwa
Akiwa ni miongoni mwa wanainchi wachache waliobahatika kupata elimu ya kupiga vita masuala ya ukeketaji Wilayani Tarime kutoka katika shirika la Pact Tanzani ambalo limekuwa likiendesha semna na mafunzo ya kupambana na ukeketaji Wilayani Tarime, Zephania Mwita Mang’ache anasema kwamba amebadilika sana kimtizamo na ametokea kuichukia mila hiyo ya ukeketaji.

“Mimi hii elimu ya kupambana na ukeketaji nimebahatika kuipata katika
NGO’s moja hivi inayoitwa Pact; kiukweli Pact wamenisaidia sana kupata uelewa wa masuala haya ya ukeketaji, hivyo ningeshauri na mashirika mengine yaanze kutoa ulimu kama hii hapa Wilayani hususani kwa wazee wa kimila na mangariba kwa kuwa wao ndio wanaosimamia zoezi hili la ukeketaji” alisema.

Lakini jambo la kufurahisha ni kwamba baadhi ya wazazi Wilayani Tarime wamechukua hatua mapema ya kupambana na ukeketaji kwa mabinti zao, hatua ambayo imekuja si tena kwa kupata elimu ya kupambana na ukeketaji, la hasha!, bali hatua hiyo imetokana na madhara waliyoyashuhudia awali wakati wakiwafanyia ukeketaji mabinti zao.

Mama mmoja kutoka Kijiji cha Kenyamanyori Wilayani Tarime ambae ana watoto wa kike watatu anaeleza kwamba baada ya kumfanyia ukeketaji binti yake wa kwanza, alitokwa na damu nyingi hadi kumpa wasiwasi wa binti huyo kupoteza maisha, hali iliyosababisha kuuchukia ukeketaji na hivyo kuamua kutowafanyia ukeketaji mabinti zake wawili waliosalia.

“Mimi huyu binti wangu wa kwanza nilipomfanyia ukeketaji alitokwa na damu nyingi hadi nikahofia kumuongezea damu huyu motto” alieleza tena kwa uchungu mkubwa huku akiwashauri wananchi wa Tarime kubadilika na kuachana na mila hiyo ya ukeketaji.

Lakini simanzi, kilio na majonzi yasiyo futika bado yanazidi kuwaumiza wahanga wa janga hili la ukeketaji, haswa kutoka na baadhi yao kufanyiwa ukeketaji kwa kulazimishwa na wazazi wao bila hiari yao, huku madhara wanayoyapitia maishani mwao yakizidi kuwaumiza mioyoni mwao kila wanapoukumbuka unyama waliotendewa.

Aikiwa ni miongoni mwa wanawake waliofanyiwa ukeketanji katika enzi za utoto wake, anaeleza kwamba haikuwa hiari yake kufanyiwa ukeketaji bali alilazimishwa na wazazi wake, huku wakimtishia kuwa wangelimfukuza nyumbani kama asingelikubaliana na uamuzi huo.

“Haikuwa hiari yangu bali nililazimishwa na wazazi wangu; tena waliniambia nikikataa kutahiriwa watanifukuza nyumbani kwa sababu wao hawawezi kukaa na binti ambae hajakeketwa; ikabidi nikubali; lakini ni kitendo ambacho nakilaani na siwezi kumfanyia hata binti yang; mbaya zaidi wakati nakeketetwa nilikuwa na umri wa miaka 14 na nilitokwa na damu nyingi sana” alisema mwanamke huyo.
MTANZANIA MEDIA: ITAENDELEA...

No comments:

Powered by Blogger.