LIVE STREAM ADS

Header Ads

AJALI MBAYA YATOKEA MANYONI MKOANI SINGIDA, IKILIHUSISHA BASI LA ZUBERY NA GARI DOGO LA ABIRIA.

Hili ni gari dogo la Abiria ambalo limegongana Uso kwa Uso na Basi la Zubery katika Eneo la Manyoni Mkoani Singida ikilihusisha basi la Zubery linalofanya Safari zake katika Mikoa ya Dar es salaam na Mwanza. Ajali hiyo imetokea Mchana huu majira ya Saa Nane ikitokea Jijini Dar kuelekea Mkoani Mwanza.
Mpaka sasa hakuna taarifa za uhakika kama kuna abiria wamepoteza maisha katika ajali hii mbali ya kusababisha majeruhi takribani wote waliokuwa katika gari hili dogo la Abiria.
Basi la Zubery ambalo limepata ajali mchana huu majira ya saa nane kwa kugongana uso kwa uso na gari dogo la abiria katika eneo la Manyoni Mkoani Singida.Katika Basi hili Abiria hajadhurika Hivyo ni jambo la Kumushukuru Mungu.
Picha zote na Dk.Tonny @Radio Metro kwa ushirikiano na Antony Marcus (Mdau).

No comments:

Powered by Blogger.