LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAASKARI KK-SECURITY WAZUNGUMZA HALI HALISI ILIVYO.



Wahitimu wa Mafunzo ya Ulinzi na Usalama Kutoka Kampuni ya Ulinzi ya KK-Security Group Wameyashauri Makampuni binafsi ya Ulinzi hapa nchini, kutoka ndani na Nje ya nchi kuhakikisha yanaajiri Maaskari wenye ujuzi na Mafunzo ya Ulinzi na Usalama tofauti na ilivyo kwa baadhi ya Makampuni binafsi ya ulinzi ambayo huajiri Maaskari wasio na Ujuzi.

Wahitimu hao waliyasema hayo jana katika Uwanja wa Nyamagana Mkoani Mwanza, baada ya kuhitimu mafunzo yao ambayo hutolewa na KK-Security, ambapo walibainisha kuwa kampuni ya ulinzi kumuajiri askari asie na ujuzi wowote na kazi hiyo kunahatarisha usalama wake sanjari na eneo husika analolinda kwa ujumla.

Aidha waliyashauri Makampuni binafsi ya Ulinzi hapa nchini kuhakikisha yanazingatia suala la Maslahi bora na yanayotolewa kwa wakati kwa maaskari wake ili kuondoa vishawishi vinavyoweza kuwakumba maaskari wawapo kazini kutokana na kukabiliwa na Ukata.


“Baadhi ya Kampuni ambazo zinaajiri watu bila Mafunzo, huo unakuwa sio weledi kwa sababu unampo mpeleka mtu kufanya kazi asiyoifahamu unakuwa umemuingiza kwenye mambo ambayo hayafamu na unamuweka katika hatari ya kuingia katika lhasara kwa Kuibiwa na kujikutana akiharibu kazi…” Walisema Wahitimu hao.

Kuhusu Maslahi kwa Maaskari kutoka kampuni binafsi za Ulinzi,Maaskari Wahitimu hao walisema kuwa maslahi duni kwa maaskari yasipoepukika yanaweza kuhatarisha utendaji kazi wao kwa kuwa askari asipolipwa vizuri na kwa wakati anaweza kujiingiza katika vitendo vya kushirikiana na waharifu na hivyo kuhatarisha utendaji kazi wa kampuni husika.


Kampuni ya KK-Securiti imekuwa na Utaratibu wa Kuandaa Mafunzo kwa Maaskari wake wa Ulinzi kabla ya Kuwaajiri ambapo katika zoezi hili Mafunzo yamekuwa yakitolewa kwa awamu mbalimbali  huku Mkoa wa Mwanza ukiwa ni Moja ya Vituo vya Mafunzo  vya Kampuni hiyo Kwa ajiri ya Kuwafunza mbinu mbalimbli za Ulinzi na Usalama Maaskari wake jambo ambalo limekuwa likiimarisha utendaji kazi wa Kampuni hii na hivyo kuwa kivutio cha watu na Makampuni mengi yanayohitaji huduma ya Ulinzi.
Meneja wa Kampuni ya Ulinzi KK.Secury Kanda ya Ziwa Levina Vedasto Beal.
  Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.