USICHOKIJUA KUHUSU SHOW YA SERENGETI FIESTA 2014.
Dakika chache mara baada ya Ratiba ya Serengeti Fiesta 2014 kutangazwa
Rasmi, Homa ya Show hiyo Kubwa Kabisa hapa nchini imetanda kila kona katika
Mikoa ya Kanda ya Ziwa, hususani kwa wakazi wa wananchi wapenda burudani wa
Jiji la Mwanza.
Muda mfupi tu mara baada ya Ratiba ya Serengeti Fiesta
Kutangazwa hii leo kupitia Kipindi cha XXL Kinachorushwa na Clouds FM na Mwenyekiti wa kamati ya
Fiesta 2014 Sebastian Maganga, nilipigwa na butwaa kwa wapenzi wa burudani niliokutana nao katika
viunga vya Jiji la Mwanza ambao kila mmoja aliielezea show hiyo kwa mwonekano
wa kuisubiri kwa hamu kubwa.
Kilichochsababisha pia nikapigwa na Butwaa ni pale wapenzi wa
Burudani waliposhindwa kuficha hisia zao na kuonekana kufurahishwa na Ratiba za
Fiesta 2014 kuanzia Kanda ya Ziwa ambapo show ya kwanza itapigwa katika Dimba
la CCM Kirumba tarehe 09 Mwezi wa Nane mwaka huu (09.08.2014) kwa kiingilio cha shilingi 5,000 tu.
Siku moja kabla ya Kutangazwa kwa Show hiyo ya Fiesta (Jana
Jumatano) Nilikutana na Baaadhi ya Wasanii wa Jiji la Mwanza, kiukweli
nilishangwa na namna kila mmoja alivyokuwa akinieleza kuhusiana na Serengeti Fiesta 2014.
Wengi walinieleza namna ambavyo wamekuwa wakijifungia Studio ili kuhakikisha
wanatoka na ngoma kali ambazo zitawapa nafasi ya kupanda katika Jukwaa la
Fiesta 2014.
Baada ya Kuwasikiliza kwa Makini Wasanii hao, ndipo
nikagundua Utofauti kati ya Shows zote ambazo zinapigwa hapa nchini. Kwanza kwa
mapokeo tu ya wapenzi wa Burudani Jijini Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla
walivyoipokea Show hii, lakini pia namna ambavyo Wasanii wa Mwanza
walivyonieleza kuwa wanaumiza vichwa ili kuhakikisha wanapata fursa ya kupanda
katika Jukwaa la Fiesta Mwaka huu.
Kwa Mantiki hiyo, nadiriki kusema kuwa huu ndio utofauti kati
ya Show ya Serengeti Fiesta na Shows zote hapa nchini ambapo hii inaashiria kwamba
shughuli yoyote ile katika jamii ni MAPOKEO. Kama shughuli ina mapokeo HASI
katika jamii basi hiyo shughuli unaachana nayo na kuangalia shughuli nyingine
ya kufanya ambayo itakuletea mapokeo CHANYA katika Jamii.
Hadi kufikia hapa naweza kutamatisha kwa kusema kuwa SERENGETI FIESTA
imeonyesha mapokea CHANYA katika jamii kwa maana ya wapenzi wa Burudani na
Wasanii kwa ujumla hivyo ni jukumu la wahusika kuendelea kuiboresha Show hii
ili imani ya wapenda burudani hapa nchini iendelee kuwepo ikiwa ni pamoja na
wasanii wenyewe ambao tayari wamekuwa na Imani kwamba, wakipanda katika Jukwaa
la Fiesta basi wanakuwa wamepiga hatua moja wapo kubwa ya Kimafanikio katika
mziki wao.
HII NDIYO RATIBA KAMILI YA FIESTA 2014
Na Mhariri: Mtanzania Media Blog.
No comments: