LIVE STREAM ADS

Header Ads

KK SECURITY GROUP KUNANI?

Wahitimu wa Mafunzo ya Ulinzi na Usalama Kutoka Kampuni ya KK Security. Kampuni hii ina Utaratibu wa Kutoa Mafunzo kwa Maaskari wake kabla ya Kuwaajiri, jambo ambalo linapaswa kuigwa na Kampuni nyingine za Ulinzi kutoka ndani na nje ya Nchi.Hii ilikuwa leo Katika Uwanja Mkongwe wa Nyamagana Mkoani Mwanza. UTOAJI WA MAFUNZO KWA MAASKARI WA KK SECURITY KUNANIFANYA KUULIZA "KK SECURITY KUNANI? MBONA NYIE JAMBO HILI MMELIMDUMU? KAMPUNI NYINGINE MNASHINDWA NINI? NA MATOKEO YAKE MNAAJIRI MAASKARI KIENYEJI ENYEJI"? KAMA KUNA KAMPUNI NYINGINE INAYOFANYA HIVI BASI INASTAHILI PONGEZI, LAKINI NIJUAVYO KAMPUNI NYINGI ZINAAJIRI KWA KUOKOTEZA OKOTEZA. KWA HILI JIFUNZENI. NA KAMA SI KUTOA MAFUNZO, BASI AJIRI MTU AMBAE AMEPITIA MAFUNZO YA JWTZ, JKT, MGAMBO NK. Tazama Picha zote kuhusiana na kilichojili katika Uwanja huo wa Nyamagana.
"Jamaa wako Vizuri, Kiukweli KK Security ni Mfano wa Kuigwa. Sio kama Kampuni nyingine ambazo zinaajiri tu bila kutoa Mafunzo kwa Maaskari wake hali ambayo ni hatari kwa kuwa unamuajiri mtu kufanya kazi ambayo haijui jambo ambalo linahatarisha utendaji kazi" Alieleza Mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo hayo Wakati akizungumza na Mtanzania Media.
Hapa walikuwa wakionyesha namna ya Kupambana na Adui na Kumuweka chini ya Ulinzi.
Meneja wa Kampuni ya Ulinzi KK.Secury Kanda ya Ziwa Levina Vedasto Beal.
Ahsante kwa kutembelea Mtanzania Media, Jiunge nasi Mara kwa Mara kwa Habari, Picha na Matukio Mbalimbali. Mtanzania Media, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii.
Na: George Binagi @Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.