LIVE STREAM ADS

Header Ads

MBIO ZA ROCK CITY MARATHON KUTIMUA MBIO JUMAPILI OCTOBA 26 MWAKA HUU MKOANI MWANZA.

Mratibu wa mbio za Rock City Marathon Methew Kasonta (Kushoto) akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Rock City Marathon Mkoa wa Mwanza Gibson Mtaegea (Kulia).
Mashindano ya Riadha  ya Rock City Marathon yanatarajia kufanyika Oktoba 26 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba yakiwa yanafanyika kwa mara ya sita mwaka huu.

Akizungumza
juzi na wandishi wa habari za michezo wa Mkoa wa Mwanza, Mratibu wa mbio hizo kutoka Kampuni ya CAPITAL PLUS INTERNATION Methew Kasonta alisema kuwa mwaka huu katika mbio hizo kutakuwa na mashindano katika mbio za km 12, km5 kwaajili ya makampuni na walemavu wa ngozi(albino) km3 kwaajili ya wazee,  km2 kwa ajili ya watoto  pamoja na mbio fupi za uwanjani mita 100, mita 400 na mita 1500.

Aidha Kasonta alisema kuwa mshindi wa kwanza katika mbia za km12 atapata zawadi ya sh. ml 1 na laki 5, mshindi wa pili laki tisa, mshindi wa tatu laki 7, mshindi wa nne na wa tano laki 1 huku wa sita hadi kumi wakipata elfu hamsini ambapo katika mbio za km5 msindi wa kwanza atapata Tsh 50,000/= wa pili 30,000/= na wa tatu 20,000/=.

Kasonta aliendelea kusema msindi wa kwanza katika mbio za km 3 maalum kwa wazee na km3 kwa watoto atapata Tsh. 50,000/= Wa pili 30,000/=  wa tatu 20,000/= huku wa nne hadi wa kumi  akipata shilingi 10,000/=.

Katika mbio fupi za uwanjani mita 100 mshindi wa kwanza atapata Tsh 40,000/= wa pili 25,000/= wa tatu 15,000/= na kwenye mbio za mita 400 mshindi wa kwanza atapata 40,000/= wa pili 25,000/= wa tatu 15,000/= na katika mita 1500 wa kwanza atapata 40,000/= wapili 25,000/= na wa tatu 15,000/=.

Akiyataja maeneo yatakayopitiwa katika mbio hizo mjumbe wa kamati ya Rock City Marathon Mkoa wa Mwanza Gibson Mtaegea alisema  kuwa mbio za km 21 zitaanzia uwanja wa CCM Kirumba hadi kwenye mzunguko wa samaki, mbio za km5 zitaanzia Mabatini hadi CCM Kirumba,  mbio za km3 zitaanzia Makaburi ya wahindi (Mt.meru Filling Station) hadi CCM Kirumba wakati mbio za watoto za km2 zitaanzia Mwaloni hadi CCM Kirumba.

Mtaegea alisema kuwa fomu za ushiriki katika mbio hizo zinapatikana katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza huku akibainisha kwamba gharama za upatikanaji wa fomu hizo kuwa ni Tsh 5,000/=  katika mbio za km 12, shilingi 3,000/= km3 na shilingi 2,000 kwa km 2.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania Suleyman Nyambui aliwataka wakazi wa Jiji la Mwanza kushiriki kwa wingi katika mchezo huo kwa kuchukua fomu ama kujitokeza kwa wingi siku ya tukio kwa ajili ya kuwashangilia washiriki na kuwatia moyo kwani kwa kufanya hivyo pekee kutatia hamasa na kuendeleza mchezo wa riadha na kuufanya upige hatua kama ilivyo katika Mkoa wa Kilimanjaro ambao umeendelea sana katika riadha.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania Suleyman Nyambui .
Na:Jacktan Msafiri.

No comments:

Powered by Blogger.