LIVE STREAM ADS

Header Ads

ANYWESHWA MKOJO ILI KUNUSURU MAISHA YAKE BAADA YA KUBUGIA GONGO.

Kijana mwenye nguo yenye rangi nyekundu kwenye pikipiki akiwa hoi baada ya kubugia pombe haramu ya Gongo tayari kwa ajili ya kukimbizwa Hospitalini kwa ajili ya kupata huduma.Hapa kijana huyu amekwisha patiwa huduma ya kwanza na wanazengo hawa kwa KUMNYWESHA MKONYO kwa ajili ya kupunguza makali ya pombe hiyo ambayo imemuacha hoi hajitambui.
Kijana mmoja aliefahamika kwa jina moja la Mtanzania amenusurika Kifo baada ya kukutwa akiwa taabani kutokana na kubugia pombe haramu ya Gongo.

Tukio hilo limetokea
wiki iliyopita Wilayani Tarime Mkoa wa Mara baada ya Kijana huyo akiwa na wenzake kufika katika nyumba moja maarufu kwa kuuza pombe haramu ya Gongo iliyopo katika Kijiji cha Rebu Kata ya Turwa nje kidogo kutoka Tarime Mjini kwa ajili ya kupata kinywaji hicho.

Wakielezea tukio hilo, wananzengo wa Kijiji cha Rebu walidokeza kwamba, akiwa na wenzie kijana huyo alifika katika nyumba hiyo maarufu kwa kuuza gongo majira ya jioni kwa ajili ya kupata kinywaji cha gongo ambapo aliitandika ipasavyo kiasi cha kumfanya azidiwe na kuzima kabisa (Kuzirahi).

Baada ya kijana huyo kuzirahi ikiwa ni majira ya usiku, wateja wengine waliokuwa nae walimmbeba kutoka katika nyumba hiyo na kumtelekeza katika darasa la shule ya awali liliyopo mita chache kutoka katika nyumba hiyo ya kuuzia gongo huku lengo likielezwa kuwa ni kupoteza ushahidi endapo kama kijana huyo angepoteza maisha.

Ilipofika asubuhi wanazengo waliokuwa wakibugia gongo na kijana huyo walifika katika eneo walilokuwa wamemtelekeza na kukuta bado anapumua japo mbali huku bado akiwa hajitambui, ambapo mipango ya kumpatia huduma ya kwanza ilianza mara moja ambapo alijitokeza msamalia mwema na kutoa mkojo wake kwa ajili ya kijana huyo kunywesha kwa lengo la kupunguza makali ya gongo mwilini huku wengine wakikimbilia maziwa kwa ajili ya kumnywesha.

Baada ya Kijana huyo kunywesha Mkojo, bado hakupata nafuu na juhudi za kumkimbiza Hospitalini zilianza mara moja, ambapo alikimbizwa katika Hospitali moja Mjini Tarime kwa ajili ya kupatiwa huduma zaidi.

Mtanzaniamedia Blog ilipozungumza na baadhi ya wananchi waliokuwa katika eneo la tukio walieleza kwamba, nguvu kazi Wilayani Tarime inaelekea ukingoni kutokana na Wananchi wengi wazee kwa vijana kutumbukia katika wimbi la unywaji wa pombe haramu ya gongo na uvutaji wa bangi licha ya kuwepo kwa mapambano ya kuzuia ulimaji na uvutaji wa bangi sanjari na utengenezaji na unywaji wa Gongo walioeleza kuwa unafanywa na polisi Wilayani humo.

Wengine walienda mbali zaidi na kueleza kwamba mapambano ya kuzuia ulimaji na utengenezaji wa bangi pamoja na utengenezaji na unywaji wa pombe haramu ya gongo bado ni kitendawili Wilayani Tarime kutokana na juhudi za polisi kuonekana kukwamishwa na mkono wa umate umate kutoka kwa washukiwa wa biashara hizo.
TAZAMA PICHA ZA TUKIO ZIMA.
Kijana (mwenye nguo nyekundu) akiwa hoi hajitambui baada ya kufakamia pombe haramu ya gongo.
Wananzengo w akijadiliana kwa ajili ya kumfikisha hospitalini.kijana aliebugia gongo.
"Hakika Gongo si Maji"
Safari ya kumpeleka kijana huyo aliebugia pombe haramu ya gongo ikaanza. Lakini nikujuze tu kwamba baada ya siku tatu Mtanzaniamedia Blog ikadokezwa kwamba kijana huyo alifanikiwa kupata matibabu na kuruhusiwa kutoka Hospitalini, na juhudi za kumsaka ili kuongea nae hazikuweza kufanikiwa.
Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.