LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAHAFALI YA 13 KIDATO NNE MKOLANI SEKONDARI JIJINI MWANZA YATIKISA JIJI.

Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha nne Sule ya Sekondari Mkolani iliyopo Kata ya Mkolani Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza wakiwa Ukumbini ikiwa ni katika Mahafali ya 13 ya Kidato cha nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 1999.Mahafali hayo yalifanyika jana Octoba 24.2014 katika Ukumbi wa Shule hiyo.
Mahafali ya 13 ya Kidato cha nne mwaka 2014 Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza yameacha historia kubwa kwa wanafunzi, waalimu, wazazi na wageni wote waalikwa walioshuhudia Mahafali hayo kutokana na
namna yalivyofanyika.

Mahafali hayo ambayo yalifanyika jana katika Ukumbi wa Shule hiyo yenye kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Sita, yalionekana kuwa ya tofauti kutokana na namna yalivyoandaliwa kutokana na Manjonjo mbalimbali yaliyoonyeshwa na wanafunzi wa shule hiyo ambao ni waaga na waagwa.

Miongoni mwa mambo yaliyoonekana kuwavutia wale wote walioshuhudia Mahafali hayo ni pamoja na burudani mbalimbali zilizotolewa na wanafunzi wa shule hiyo, burudani ambazo ni pamoja Kucheza nyimbo za asili, nyimbo za kisasa, Maonyesho ya Mitindo (Mavazi) ikiwa ni miongoni mwa mambo mengine mengi ya kiburudani.

Akizungumza katika Mahafali hayo, Mkuu wa Shule hiyo Mwl.Asensio Mathias aliwataka wanafunzi wanaotarajia kuhitimu masomo yao mwaka huu kuutumia vyema muda mfupi uliosalia katika kujiandaa vyema na mtihani wao wa mwisho unaotarajia kuanza Novemba 03 Mwaka huu.
Wahitimu wakiwa Ukumbini.
Mwl.Mathias aliwasihi wanafunzi hao kuongeza juhudi zaidi ili kuiweka shule hiyo katika nafasi nzuri ya ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne, tofauti na ilivyokuwa mwaka jana ambapo shule hiyo ilishika nafasi ya 90 kati ya shule 204 katika Mkoa wa Mwanza, huku Kitaifa ikishika nafasi ya 1,345 kati ya Shule 3,256.

Nae Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo, Diwani wa Kata ya Mahina (Chadema) Charles Chinchibela ambae alimwakilisha Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje (Chadema), alisema kuwa ili kuongeza kasi ya ufundishaji na hatimae ufaulu kwa wanafunzi, lazima waalimu waanze kupewa Motisha mbalimbali pale ambapo wanafunzi watakuwa wakifaulu vyema katika masomo ambayo wanayafundisha.

Kuhusu changamoto zinazoikabili shule hiyo ambazo zilibainishwa katika Risala iliyosomwa na wanafunzi wanaotarajia kuhitimu kidato cha nne mwaka huu, Chinchibela alibainisha kuwa ataziwasilisha kwa Mh.Mbunge kwa lengo la kuangalia namna ya kuzitafutia ufumbuzi.

Miongoni mwa changamoto zilizobainishwa katika Risala ya wahitimu mbele ya mgeni Rasmi ni pamoja na ukosefu wa Wigo katika Shule hiyo sanjari na katika Mabweni ya wasichana wa kidato cha Tano na Sita Shuleni hapo.

Takribani Wanafunzi 98 wa Kidato cha nne katika Shule hiyo ya Mkolani iliyopo Kata ya Mkolani Jijini Mwanza, wanatarajia kuhitimu kidato cha nne mwaka huu, ambapo wanafunzi hayo waliieleza Mtanzaniamedia Blog kwamba wamejiandaa vyema katika mtihani wao wa mwisho hivyo wanatarajia ufaulu bora kutokana na ufundishaji mzuri walioupata kutoka kwa waalimu wao na hata nje ya waalimu wao.
Wahitimu wakiingia Ukumbini.
Wahitimu wakiruka Majoka.
Wanafunzi wakionyesha ubunifu wa mavazi mbalimbali ambapo ni pamoja na Vazi la Shuleni, Kanisani,Msikitini, Ofisini, Udakitali, Vazi la Kitenge, Vazi la Askari nk.
Wanafunzi wakionyesha ubunifu wa mavazi mbalimbali ambapo ni pamoja na Vazi la Shuleni, Kanisani,Msikitini, Ofisini, Udakitali, Vazi la Kitenge, Vazi la Askari, Vazi la Baba na Mama Afrika nk.
Wanafunzi wakionyesha Umahili katika kucheza nyimbo za kisasa.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkolani wakishuhudia burudani...Hawa ni Waaga.
Baadhi ya Wazazi na Walezi waliofika katika Kushuhudia Mahafali ya 13 Kidato cha nne Mkolani Sekondari.
Taswira ya Ukumbi ilivyokuwa kutoka nyuma.
Baadhi ya Wazazi na Walezi waliofika katika Kushuhudia Mahafali ya 13 Kidato cha nne Mkolani Sekondari.
Baadhi ya Waalimu wa Shule ya Sekondari Mkolani.
Baadhi ya Waalimu wa Shule ya Sekondari Mkolani.
Wageni (Waalimu) Waalikwa kutoka Shule Jirani.
Waalimu wa Taaluma (Wawili kushoto) kutoka Mkolani Sekondari, Wa kwanza Kulia ni Mwakilishi wa Mgeni Rasmi Charles Chinchibela ambae ni Diwani wa Kata ya Mahinda (Chadema).Chincibela alimwakilisha Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Hezekiel Wenje (Chadema).
Waalimu wa Mkolani Sekondari wakiwakabidhi Keki Wanafunzi wa Kidato cha nne wanaotarajiwa kuhitimu mwaka huu.
Mwalimu wa darasa akielezea mapenzi yake kwa wahitimu sanjari na kuwakabidhi keki aliyowaandalia kama ishara ya upendo wake kwao.
Hiyo ni kadi yenye Majina yote 98 ya wanafunzi wa kidato cha nne Mkolani Sekondari ambayo wanatarajia kuhitmu mwaka huu.
Kumbuka Mwl.Isaack Wakuganda (Wa Kwanza Kulia) kutoka Mkolani Sekondari ndie alikuwa MC wa Shughuli.Wakuganda pia ni Mwandishi na Mtangazaji Mahiri wa Habari za Michezo, na Habari/Vipindi mbalimbali pia.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari akizungumza jana katika Mahali ya kidato cha nne shuleni hapo.
Wa kwanza Kushoto ni Mgeni Rasmi Mh.Charles Chinchibela ambae ni Diwani wa Kata ya Mahina (Chadema) akisaini kitabu cha wageni na Kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkolani Mwl.Asensio Mathias.
Wa kwanza Kushoto ni Mgeni Rasmi Mh.Charles Chinchibela ambae ni Diwani wa Kata ya Mahina (Chadema).
Taswira Meza Kuu.
Mmoja wa Wahitimu akipokea Cheti kwa ajili ya Ukumbusho.
Kumbukumbu kidogo na Mwanafunzi wa Kidato cha nne ambao aliongoza kwa ufaulu wa Masomo katika kipindi chote cha Miaka Minne.
Kumbukumbu zikiendelea.
Kumbukumbu zikiendelea.
Wahitimu wakisoma Risala yao Mbele ya Mgeni Rasmi.
Misosi nayo ilikuwepo na ilinogeshwa na Swai Catering.
Kwenye Music alisimama vyema Dj Hussein na wenzie kutoka Ratino Sound. KAMA NAWE UNAPENDA SHUGHULI YAKO IONEKANE KATIKA MTANDAO HUU PIGA SIMU NAMBARI 0757 43 26 94...MTANZANIAMEDIA BLOG-KWA PAMOJA, TUIJUZE JAMII.
Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.