LIVE STREAM ADS

Header Ads

MDAHALO JUU YA DAWA ZA KULEVYA WAFANYIKA JIJINI MWANZA.

Meneja wa Kituo cha Ushauri na Saha juu ya Masuala ya Dawa za Kulevya SOBA HOUSE Pasiansi Mohamed Abdallah Mohamed (Wa kwanza kulia), akifuatiwa na Edwin Soko ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wanaopiga Vita Matimizi ya dawa za kulevya na uhalifu nchini OJADACT, huku mwenye Kinasa Sauti akiwa ni Benard James ambae ni Mtangazaji kutoka Sahara Communication ambapo wa Kwanza Kushoto ni Adam Rajabu ambae ni Mshauri wa Dawa za Kulevya kutoka Shirika la ICAP.

Hii ilikuwa katika Mdahalo uliofanyika juzi Jumamosi Oktiba 25.2014 katika Hotel ya Pegion Jijini Mwanza ukiangazia katika Masuala ya Dawa za Kulevya ambayo Mada kuu ilikuwa ni Kwa nini Dawa za Kulevya (Why Drug Abuse) ambapo Wadau mbalimbali waliweza kushiriki katika Mdahalo huo na kutoa mawazo yao ambayo yatasaidia katika kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya hapa nchini.Wadau hao ni pamoja na Wanahabari, Walioacha matumizi ya dawa za kulevya, Maafisa wa polisi sanjari na washauri mbalimbali wa kuhusiana na matumizi ya dawa za kulevya.Unaweza kutazama kilichojili katika Mdahalo huo kupitia Star Tv siku ya Alhamisi saa tisa na Nusu Alasiri katika kipindi cha Hoja Yangu.Mdahalo huo uliandaliwa na OJADACT kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali. TAZAMA PICHA ZA MDAHALO HUO.
Ahsante kwa kuungana na MTANZANIAMEDIA BLOG kila siku.Kwa Pamoja, Tuijuze Jamii.
Na:George Binagi.

1 comment:

Powered by Blogger.