LIVE STREAM ADS

Header Ads

MATUKIO YA KUVUTIA KATIKA PICHA KWENYE MBIO ZA ROCK CITY MARATHON 2014 JIJINI MWANZA.

Washindi wa nafasi ya Kwanza hadi ya Tatu katika Mbio za Kilomita 21 wanaume katika Mashindano ya Rock City Marathon 2014 yaliyofanyika Mkoani Mwanza Jumapili ya Octoba 26 wakichukua zawadi zao. Mashindano hayo
huandaliwa na Kampuni ya Capital Plus.
Mshindi wa Kwanza wa Kilomita 21 katika Mbio za Rock City Marathon 2014 Joseph Panga kutoka Manyara nchini Tanzania akichukua Zawadi baada ya kuibuka mshindi wa mbio hizo kwa kutumia muda wa saa 01:02:30.Mbio hizo zilianzia Uwanja wa CCM Kirumba na kupita katika mzunguko wa Samaki na kwenda hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kisha kurudi katika Uwanja wa CCM Kirumba.Panga alijinyakulia shilingi Milioni Moja na Laki Tano.
Washindi wa mbio za Kilomita 21 Wanaume katika Mashindano ya Rock City Marathon 2014 wakiwa katika picha ya Pamoja na Endrew Mtaka ambae ni Rais wa Shirikisho la Riadha nchini (RT) wa tatu pande zote pamoja na Hamis Fakii ambae ni Meneja Kiongozi kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Mwanza (Wa kwanza Kushoto).NSSF ndiyo walikuwa wadhamni wakuu wa mbio hizo. Washindi wa mbio hizo ni Joseph Panga kutoka Manyara Tanzania (Wa pili kushoto) ambae alishika nafasi ya kwanza kwa kutumia mda wa saa 01:02:36, mshindi wa pili ni Sammy Nyokaye kutoka Kenya (wa pili kulia) ambae alitumia saa 01:02:39 na mshindi wa tatu akiwa ni Festus Talam nae kutoka Kenya (wa kwanza kulia) ambae alitumia saa 01:15:34.
Watoto wakipokea zawadi baada ya kuibuka washindi.
Mshindi wa kilomita tatu wazee kwa upande wa akina mama akipokea zawadi yake. 
Washindi wa Mbio za kilomita 21 wanawake wakiwa katika picha ya pamoja.Washindi hao ni Mathalia Elisante (wa tatu kulia) ambae alitumia muda wa saa 01:14:25, akifuatiwa na Mary Naali (wa tano kulia) alietumia muda wa saa 01:15:34 pamoja na mshindi wa tatu ambae ni Adelina Audata (wa pili kushoto) ambae alitumia muda wa saa 01:23:01. Zawadi kwa washindi hao ni shilingi Milioni Moja na Laki Tano kwa mshindi wa kwanza, shilingi Laki Tisa Mshindi wa Pili na shilingi Laki Saba Mshindi wa Tatu.
Andrew Mtaka ambae ni Rais wa Shirikisho la Riadha nchi RT (aliesimama kushoto) akizungumza katika mashindano ya Rock City Marathon 2014 yaliyofanyika jumapili ya Octoba 26 mwaka huu Mkoani Mwanza.
Hamis Fakii ambae ni Meneja Kiongozi kutoka NSSF Mwanza (kushoto) akizungumza katika kilele cha mashindano ya Rock City Marathon 2014.NSSF walikuwa wadhamni wakuu wa mashindano hayo mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Amina Masenza (Mwenye kinasa sauti) akitoa hotuba yake kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo katika Mashindano ya Rock City Marathon 2014.
Hamis Salehe ambae ni Meneja wa Bank ya CRDB Mwanza (Kulia) akizungumza na Jacob Marcus (kushoto) kuhusiana na Mashindano ya Rock City Marathon 2014.Bank ya CRDB ni miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza kudhamini mashindano hayo.
Hamis Fakii ambae ni Meneja Kiongozi kutoka NSSF Mwanza (Kulia) akizungumza na Jacob Marcus (Kushoto) Kutoka Star Tv juu ya Mashindano hayo.NSSF ndio walikuwa wadhamni wakuu wa mashindano hayo mwaka huu.
Mshindi wa Kwanza wa Mbio za Kilomita 21 wanawake Mathalia Elisante (Kushoto) kutoka Tanzania akizungumza na Jacob Marcus kutoka Star Tv (Kulia). Elisante alitumia musa wa saa 01:14:25 kuweza kumaliza mbio hizo.
Mratibu wa Mashindano ya Rock City Marathon Mathew Kasonta akizungumzia mashindano hayo ambao alisema yamelenga kuinua mchezo wa Riadha hapa nchini.
Kutoka Uwanja wa Mabatini na sasa wamefika Mtaa wa Rufiji kuelekea Uwanja wa CCM Kirumba ambapo hizi ni mbio za kilomita tano.
Aliibuka Mshindi wa Kilomita 5 lakini kwa bahati mbaya alishiriki bila kujua kwamba mbio hizi kwake hazikuwa na zwadi.Maana kwa mbio za kilomita Tano, walemavu wa ngozi ndio waliopata zawadi.NB:Ni vyema kusoma Vigezo na Masharti kabla ya kushiriki katika jambo lolote maana huyu bwana alitoka Mkoani Arusha na alilalamika sana baada ya kukosa zawadi.
Hizi zilikuwa ni mbio za kilomita Tano ambazo zilianzia uwanja wa Mabatini na kuishia Uwanja wa CCM Kirumba.Katika Mbio hizi walemavu wa ngozi ndio waliopata zawadi.Wengine walikuwa wakichangamsha akili.
Mbio zikiendelea kama kawa.Na hapa Mshiriki kutoka NSSF akionyesha ushiriki wake na hii ikidhihirisha kwamba NSSF hawakushiriki tu katika Udhamni bali hata katika Kukimbiza upepo wako vizuri.
Ahsante kwa kuitembelea MTANZANIAMEDIA BLOG-Kwa Pamoja, Tuijuze Jamii.
Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.