LIVE STREAM ADS

Header Ads

WADAU WA MAJI WAPEWA SEMNA JUU YA UTENDAJI KAZI WA MFUMO WA WAGOSY MKOANI MWANZA.

Wadau mbalimbali wa Maji wakiwa katika Picha ya Pamoja baada ya Semna ya Siku Moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Vizano Jijini Mwanza ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa namna mfumo wa WAGOSY (Water Governance System) Unavyofanya kazi.Kupitia Mfumo huo, watumiaji wa
Maji (Wananchi) wataweza kuripoti taarifa mbalimbali zikiwemo za uchafu wa maji na vyanzo vyake kwa ajili ya hatua zaidi kabla ya madhara kutokea katika jamii.Mfumo huu unatarajia kuzinufaisha nchi za Ukanda wa Afrika Mashari katika Bonde la Ziwa Victoria ambapo kwa sasa uko katika Majaribio katika nchi za Tanzania na Uganda.Semna hiyo ilifanyika juzi jumatano Octoba 22.2014.
Mfumo wa Wagosy ni mfumo ambao umebuniwa na Wahitimu wa Teknolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ukiwa unatoa fursa kwa wananchi kuripoti matukio mbalimbali ya yanayoweza kujitokeza katika vyanzo vya maji ili kusaidia kufikisha taarifa mapema kwa watendaji kwa ajili ya hatua zaidi. Mfano wa matukio hayo ni Pamoja na Uchafuzi wa Vyanzo vya Maji, Moto, Migogoro wizi sanjari na matukio mengine mbalimbali yanayoweza kuhatarisha afya ya watumiaji wa maji.
Ili kutoa taarifa kupitia Mfumo huo, mtoa taarifa anapaswa kuandika neno linaloashiria taarifa anayohitaji kuitoa.Mfano kama ni taarifa ya Moto basi unaingia katika sehemu ya kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika simu na unaandika neno MOTO unaacha nafasi, kisha unaandika ujumbe wako na kuutuma kwenda nambari 0759 16 70 42.Kwa Matukio mengine mbalimbali unaandika neno TAAFIA na unaacha nafasi na kutuma kwenda namba ile ile ya 0759 16 70 42.
Miongoni mwa Wadau waliohudhuria semna hiyo ni pamoja na wanahabari, Viongozi wa serikali, Wasimamizi wa Maji (Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Mkoani Mwanza, wasimamizi wa Mazingira kutoka Nemc na Wavuvi.
Injinia Gogadi Mgwatu ambae ni Meneja Msaidizi Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoan wa Mwanza MWAUASA (Kushoto), akizungumza na George Binagi @Metro FM & Mtanzaniamedia Blog kuhusiana na namna ambavyo mfumo wa Wagosy utakavyosaidia katika kuboresha upatikanaji wa taarifa za uchafuzi wa maji na vyanzo vyake ambapo alikiri kuwa mfumo huo utaweza kusaidia upatikanaji wa taarifa hizo hivyo wananchi wautumie vyema katika kutoka taarifa za matukio wanayokabiliana nayo.
Ili kutoa taarifa kupitia Mfumo huo, mtoa taarifa anapaswa kuandika neno linaloashiria taarifa anayohitaji kuitoa.Mfano kama ni taarifa ya Moto basi unaingia katika sehemu ya kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika simu na unaandika neno MOTO unaacha nafasi, kisha unaandika ujumbe wako na kuutuma kwenda nambari 0759 16 70 42.Kwa Matukio mengine mbalimbali unaandika neno TAAFIA na unaacha nafasi na kutuma kwenda namba ile ile ya 0759 16 70 42.
SIKILIZA HAPA CHINI MAHOJIANO ALIYOFANYA GEORGE BINAGI KUHUSIANA NA MFUMO HUO WA WAGOSY.

Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.