LIVE STREAM ADS

Header Ads

SASA MWIGIZAJI WEMA SEPETU AWINDWA NA NYASA BOY.

NYASA BOY.
Mwigizaji Maarufu wa Bongo Movie hapa nchini Madam Wema Sepetu baada ya kudaiwa kutemana na Mbongo Fleva Diamond Platnumz, sasa anawindwa kwa udi na Uvumba na Kinda kutoka Jijini Mwanza Nyasa Boy.

Kinda huyo ambae pia ni
Mbongo Fleva a.k.a nae ni Msanii wa Mziki wa Kizazi hipya hapa nchini akitokea Rock City Mwanza-Mwanza ameeleza kuwa kwa Takribani Mwaka wa Pili sasa ameshindwa kuingia katika Uhusiano wa Kimapenzi baada ya Kutemana na Mpenzi wake huku akiapa kuwa hayuko tayari kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine mbali na Wema Sepetu ambae kwa muda mrefu amekuwa akimvutia Kimahaba.

Akipiga Story na 99.4 Radio Metro Fm siku ya Jana, Nyasa Boy ambae kwa sasa anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la "CHONGOROA" aliyomshirikisha Mc.Darada pamoja na D'Maradha alibainisha kuwa alianza kuvutiwa na Madam Sepetu tangu bado akiwa katika uhusiano wa Kimapenzi na Diamond Platnumz jambo ambalo lilipelekea yeye kuona kuwa ndoto yake hiyo haitaweza kutimia kutokana na makali ya Platnumz.

Hakika Kufa kufaana maana ndoto za Nyasa Boy kumpata Wema Sepetu ni kama zimerejea tena baada ya Madam huyo hutemana na mpenzi wake Diamond Platnumz ambae kwa sasa inaelezwa kuwa anatesa na Mwana dada mrembo na mwenye mkwanja mrefu kutoka nchini Uganda huku kwa upande wa Sepetu bado mambo yakiwa hayako wazi sana kwa sasa anatoka na nani fursa ambayo Nyasa Boy anataka kuitumia vyema.

Akijibu Swali kama ataweza kumudu gharama za kumgharimia Sepetu, Nyasa Boy alisema kuwa Mapenzi ya dhati hayahitaji pesa hivyo hivyo suala hilo halimuumizi kichwa kabisa, huku akiongeza kuwa kwa sababu hajawahi kuonana na Madam anatumia njia mbadala ili kuhakikisha kwamba aliyonayo moyoni yanamhikia Madam huyo.

Alibainisha kuwa miongoni mwa njia aliyopanga kuitumia katika kufikisha kilio chake kwa Sepetu ni pamoja na kuandaa wimbo ambao atauachia hivi karibuni ambapo wimbo huo utasukwa toka pande za Studio za Rock Town Records ukiwa unakwenda kwa jina la "WEMA SEPETU", wimbo ambao unaeleza kwa mapana zaidi namna anavyomhusudu Wema Sepetu huku akibainisha kuwa japo yeye ni mdogo kiumri kuliko Wema lakini hicho si kigezo cha kumfanya yeye asimpende Wema kwa kuwa wapo watu wengi ambao wanatofautiana umri lakini wanapendana na kudumu katika mahusiano yao ya kimahaba. Haya si yetu macho, ngoja tusubiri tuone mwisho wake ni nini.

Juhudi za MTANZANIAMEDIA BLOG Kumtafuta Madam Sepetu zinaendelea ili kuisikia yeye ana mtazamo gani juu ya Kinda huyu kueleza kumpenda lakini pia kujua kama tayari nafasi imeisha zibwa ama la, baada ya yeye kutemana na Mwandani wa Moyo wake Diamond Platnumz.
Mwigizaji Wema Sepetu.
SIKILIZA WIMBO WAKE WA CHONGOROA HAPA CHINI. MAONI 0759 21 19 77.

Na: George Binagi-GB Pazzo.

No comments:

Powered by Blogger.