LIVE STREAM ADS

Header Ads

OJADACT YALAANI MATUMIZI YA NGUVU YANAYOENDELEA HAPA NCHINI YANAYOFANYWA NA JESHI LA POLISI.

Viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uharifu nchini Tanzania.
TAMKO  LA  CHAMA  CHA WAANDISHI  WA HABARI  WA KUPIGA  VITA  MATUMIZI  YA  DAWA ZA KULEVYA  NA  UHALIFU (OJADACT) DHIDI YA MATUMIZI YA  NGUVU YALIYOFANYWA  NA POLISI  KWA  WAFUASI WA CUF.

CHAMA  CHA WANDISHI WA  HABARI WA KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA NA UHALIFU TANZANIA (OJADACT)   TUNACHUA NAFASI HII  KULAANI   MATUMIZI  YA 
NGUVU  YANAYOENDELEA  HAPA  NCHINI  YANAYOFANYWA    NA JESHI LA POLISI   DHIDI  YA  TAASISI  ZA KIRAIA.

NDUGU WAANDISHI WA  HABARI, OJADACT   TUNALAANI KWA NGUVU  ZOTE  MATUMIZI YA  NGUVU  YALIYOFANYWA   NA  JESHI LA POLISI  DHIDI  YA  VIONGOZI  NA WAFUASI   WA CHAMA  CHA  CUF JANUARI,27  KATIKA  JIJI LA DAR  ES SALAAMU, WAKATI WALIPOTAKA  KUANDAMANA  KWA  AJILI  YA  KUADHIMISHA  KUMBUKUMBU YA  MIAKA 14 YA MAUAJI  YA  WAFUASI WAO  YALIYOTOKEA  ZANZIBAR  WAKATI WA KUPINGA  MATOKEO  YA  URAIS .

NDUGU WAANDISHI    TANZANIA  NI  NCHI    HURU  INAYOFUATA  MISINGI  YA  KIDEMOKRASI,  KUTOKEA  KWA  VITENDO HIVI  MARA KWA MARA  VYA  MATUMIZI  YA  NGUVU  ZAIDI  KATIKA  MATUKIO  YA  KISIASA NI UKIUKWAJI WA HAKI   ZA BINADAMU.

RIPOTI  MBALIMBALI  IKIWEMO  YA  TUME  YA  HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA  BORA ZIMEKUWA  VIKILAANI MATUMIZI  YA   NGUVU KUBWA  YANAYOFANYWA NA  JESHI LA POLISI  DHIDI  YA  TAASISI   ZA KIRAIA PAMOJA NA WANANCHI.

POLISI  WAMEKUWA WAKITUMIA   SHERIA ZA KUTHIBITI  MIKUSANYIKO   VIBAYA  NA NI UVUNJIFU  MKUBWA  WA HAKI ZA MSINGI  ZA BINADAMU NA KUKIUKA KATIBA YA   NCHI  IBARA  YA  20  INAYOSISITIZA    HAKI  YA KUKUSANYIKA , KUJUMUIKA NA KUTO MAONI   SANJALI  NA SHERIA NO 15 YA MWAKA 1984 KIFUNGU  CHA  6  YA  UHURU WA KUKUSANYIKA.

SHERIA  HIZI NI ZA KIKOLONI  ZILITUMIKA  KUTHIBITI  HARAKATI ZA UKOMBOZI  KUTOKA  KWENYE  MAKUCHA  YA  UKOLONI  NI  AIBU KUTUMIA  SHERIA  HIZI KWENYE  NCHI  HURU  KAMA  TANZANIA.

NDUGU WAANDISHI  SISI  TUMEKUWA TUKIJIULIZA  KUWA, IWEJE  MIKUSANYIKO  YA  KISIASA NA KIHARAKATI  NDIYO  ILENGWE  ZAIDI  NA SI ARUSI, MAZISHI, MAKANISANI   NA MISIKITINI  ISWE  NA  TATIZO .

TUNAAMINI KUWA  JINAMIZI  LA  KAULI  YA WAZIRI  MKUU  MIZENGO  PINDA  YA  KUTAKA  POLISI  WAWAPIGE  WAHALIFU  TU NDIYO  INAYOTEKELEZWA  KWA SASA  NA  JESHI LA POLISI.
NDUGU WAANDISHI   TUMEJIONEA  KATIKA  NCHI MBALIMBALI  RAIA  WAKITUMIA  UHURU WAO WA KUANDAMANA NA POLISI  KUWALINDA  RAIA  HAO, KWA NINI  TUSIINGE  MFANO  HUO  KAMA  KWELI TUMEKOMAA  KIDEMOKRAIS.

OJADACT    TUNAPIGA  VITA  UHALIFU, NA HAYA YANAYOFANYIKA  NI  UHALIFU WA  SHERIA  ZA  NCHI KWANI  KUTUMIA  NGUVU KUNAMINYA  HAKI ZA  MSINGI KWA MUJIBU WA  SHERIA  ZA NCHI.

MAPENDEKEZO  YA OJADACT
1: JESHI  LA POLISI  LIFANYE  KAZI  ZAKE  KWA WELEDI  KWA KUWA NI TAASISI  MUHIMU  KATIKA KUSIMAMIA  USALAMA WA  RAIA  NA MALI ZA  NA  SI  KUSIMAMIA MANYANYASO  KWA  RAIA  WAKE.

2: WAZIRI  MKUU  AWAJIBIKE  KWA KAULI YAKE YA  KUHAMASISHA  RAIA   WAPIGWE  TU   NA VYOMBO  VYA  DOLA, KWA  KUWA  KAULI HIYO  IMEENDELEA  KUCHOCHEA  MATUMIZI  YA  NGUVU  DHIDI  YA  RAIA.

3: KIUNDWE  CHOMBO  KITAKACHOSIMAMIA  MAHUSIANO  BAINA   YA   JESHI  LA POLISI  NA  TAASISI  Z AKIRAIA.

4: JESHI LA POLISI  LISIPOTEZE   DIRA   NA  DHIMA  YA  KUANZISHWA  KWAKE  KWA  AJILI  YA  MSUKUMO WA KISIASA  HASA  KWA  UPANDE WA CHAMA  FULANIKAMA ILIVYOISNISHWA KWENYE  SHERIA  YA  KUANZISHWA JESHI  HILO.

5: JESHI  LA POLISI  LIWEKE  MASAA  24  YA  KUTOA  TAARIFA  YA  KUKUBALI AU KUKATAA  KUTOA  KIBALI CHA MAANDAMANO  NA SIO  KUKURUPUKA  TU  NA  KUZUIA  ILI KUOKOA  GHARAMA ZINAZOWEZA KUTOKEA  KATIKA  KUANDAA  MAANDAMANO  KWA  UPANDE  WA WAANDAAJI.

6: KUNA  UMUHIMU WA KUWA NA   MAJADILIANO  BAINA  YA  JESHI  LA POLISI , VYAMA  VYA  SIASA NA TUME  YA  UCHAGUZI  ILI  KUANZA  KUZUIA  DALILI  MBAYA  ZILIZOANZA KUJITOKEZA   KUELEKEA   KWENYE  UCHAGUZI  MKUU  WA MWAKA   WA MWEZI  OKTOBA  MWAKA  HUU.

7: NA MWISHO  TUNAMTAKA  WAZIRI  WA  MAMBO YA  NDANI YA  NCHI  KUCHUKUA  HATUA  KALI     POLISI  WOTE  WALIOHUSIKA  KUTUMIA   NGUVU  KUWADHITI  WAFUASI  WA  CUF  KWA  KUTUMIA  SILAHA ZISIZOKUBALIKA KATIKA  MIFUMO  YA  JESHI HILO  KAMA  SPANA   NA NYINGINEZO.
Edwin   Soko
Chairperson

JANUARI 29, 2015.

No comments:

Powered by Blogger.