LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIJANA WA KITANZANIA CHANGAMKIENI FURSA YA “LET’S TALK & TAKE ACTION PROJECT”.

Mdahalo wa wazi kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ibungiro ya Jijini Mwanza juu ya madhara ya utoaji mimba.
Mpango wa Kijanja kwa wajanja wa Town, Mradi Mpya unaolenga Kuzungumza na Kuchukua hatua kwa Mambo mbalimbali yanayowakumba vijana hasa katika masuala ya Ukosefu wa ajira, matumizi ya dawa za kulevya, mahusiano kati ya ukatili wa kijinsia na maambukizi mapya ya viruzi vya UKIMWI pamoja na nafasi ya Vijana katika Katiba inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania Mwaka huu 2015.

Mradi huu unaendeshwa na Shirika la
HAKIZETU lililopo Jijini Mwanza chini ya Usimamizi wa Shirika la Africa Center For Transformative And Inclusive Leadership lililopo Nairobi nchini Kenya unalenga Kuwafikia Vijana waliopo mashuleni na wasio Mashuleni na jamii nzima kwa ujumla katika Wilaya mbili za Mkoa wa Mwanza ambazo ni Wilaya ya Ilemela pamoja na Nyamagana.

Lengo kuu la Mradi huu ni kupaza sauti na kuchukua hatua madhubuti na zinazostahili katika kuhakikisha kwamba vijana na jamii nzima wanaondokana na tatizo la Umaskini wa kipato na fikra kwa kutoa elimu ya Ujasiliamali ili kuondokana na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa kwa vijana, tatizo ambalo limekuwa likipelekea vijana wengi kujiunga na kujiingiza kwenye makundi mabaya kama ya Ujambazi na Usafirishaji wa dawa za kulevya.

Pamoja na Lengo hilo, pia mradi huu unatoa elimu ya Afya na Makuzi kwa vijana ili kuondokana na maambukizi mapya ya magonjwa ya ngono kama vile UKIMWI sanjari na kuzuia mimba za mapema na utoaji mimba pamoja na kuzuia Ukatili wa Kijinsia.

Pia Mradi huu unatoa elimu ya Uraia na uongozi na kusisitiza vijana na jamii nzima kuisoma Katiba Pendekezwa na kushiriki katika Kugombea ngazi mbalimbali za uongozi sanjari na kujiandikisha kupiga kura ikiwa ni pamoja na kujitokeza kwa wingi kupiga kura za kuwachagua viongozi.
Mdahalo wa wazi katika shule ya Ibungiro. Aliesimama ni Mratibu wa Let's Lalk & Take Action Gervas Evodius.
Mradi huu utadumu katika Kipindi cha Miezi 12 ikiwa ni kuanzia Mwezi January hadi Mwezi Desember Mwaka huu 2015.

Mratibu wa Mradi huu Gervas Evodius ambae pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Mkoa wa Mwanza kutoka Shirika la HAKIZETU lililopo Mkoani Mwanza anasema kuwa Mradi huu ni jibu la matatizo mengo yanayowakumba vijana wa Kitanzania na jamii nzima hivyo ni vyema kwa vijana na jamii nzima ya Kitanzania kutumia vyema fursa hii ya kipekee katika kujadili na kuchukua hatua dhidi ya mambo mbalimbali yanayowakumba.

Evodius aliongeza kuwa "Vijana tuna nguvu kubwa na fursa za kutuondoa kwenye matatizo mbalimbali yanayotukabili ambayo baadhi yake ni Umaskini, Magonjwa, Ujinga pamoja na Matumizi ya dawa za Kulevya".
Baadhi ya washiriki wa mdahalo wa LET'S  TALK uliofanyika katika ofisi za shirika la Hakizetu Mwanza wakijadili juu ya madhara ya  magonjwa ya ngono na UKIMWI kwa vijana.
Na: Mratibu wa Mradi, na Kuhaririwa na Mhariri Mtanzaniamedia Blog. 

No comments:

Powered by Blogger.