LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI WILAYANI UKEREWE WALIA NA TATIZO LA MAJI. KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA ATOA KAULI.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwahutubia Wananchi Wilayani Ukerewe jana katika Uwanja wa Stand ya zamani Nansio. Mtaturu alikuwa na ziara ya siku mbili Wilayani Ukerewe iliyoanza jumatatu wiki hii na kuhitimishwa jana jumanne. Kesho alhamisi Mtaturu anaendelea na ziara zake katika Wilaya za Mkoa wa Mwanza ambapo anatarajia kufanya ziara ya Siku mbili Wilayani Sengerema.
 Na:George Binagi-GB Pazzo
Wananchi katika Mji wa Nansio Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza, wameiomba Serikali kuwasaidia kutatua adha ya Maji inayowakabili licha ya Mji huo kuzungukwa na Maji ya Ziwa Victoria.

Wakizungumza jana na Radio Metro katika ziara ya siku mbili ya Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Wilayani Ukerewe, wananchi hao walisema kuwa wanakabiliwa na adha ya maji ya bomba kukatika mara kwa mara hali inayowafanya kufuata maji ya ziwani umbali mrefu.

Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Mjini Nansio Wilayani Ukerewe Edward Joseph alikiri kuwepo kwa tatizo la Maji katika Mji huo ambapo ameeleza kuwa mabadiliko ya mfumo wa kulipia umeme yamechangia tatizo la ukosefu wa maji kuongezeka, baada ya kufungwa Luku katika mtambo wa kusambazia maji hali iliyosababisha gharama za uendeshaji wa mtambo huo kuongezeka kutoka takribani shilingi Milioni nne hadi Milioni Kumi kwa Mwezi.

Kutokana na hali hiyo, Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu alitoa muda wa siku 30 (mwezi mmoja) kwa Mamlaka ya Maji Mjini Nansio kwa kushirikiana na watendaji wengine kuhakikisha kwamba inatatua tatizo la Maji Wilayani Ukerewe.

Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu Wilayani Ukerewe ilianza jumatatu wiki hii na ilitamatishwa jana jumanne ambapo pamoja na mambo mengine katika Ziara hiyo Mtaturu alitembela Mashina ya chama hicho Wilayani Ukerewe, Miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Miradi ya Maji, Ujenzi wa Soko la Nansio pamoja na Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Nakatunguru na hatimae kuhitimisha ziara hiyo kwa kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Stand ya Zamani Nansio ambapo aliwataka wananchi kujiunga na CCM ambacho ni chama makini cha kisiasa hapa nchini.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa akitoa salamu zake kwa Wananchi Wilayani Ukerewe jana katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ukerewe Ally Hamis Mambile akitoa salamu kwa Wananchi Wilayani Ukerewe jana katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti akitoa salamu zake jana kwa Wananchi Wilayani Ukerewe katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (katikati) baada ya kufanya ziara katika kituo cha kusambazia maji Mjini Nansio akipokea maelekezo kutoka kwa Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Mjini Nansio Wilayani Ukerewe Edward Joseph (Kulia) kutokana na tatizo la Maji Wilayani humo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu pia alifanya ziara katika Soko jipya la Mjini Nansio.Bado halijaanza kutumika.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza ikitazama vyuma vitakavyotumika kwa ajili ya kulaza Mabomba ya Maji katika Mradi wa Maji Vijijini katika Wilaya ya Ukerewe.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza ikikagua tank la Maji lililojengwa kwa ajili ya kutumika kusambazia maji katika Mradi wa Maji Vijijini Unaotekelezwa chini ya Ufadhiri wa Bank ya Dunia Wilayani Ukerewe.
Charles Robert  ambae Katibu wa Shina la Wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi CCM Tawi la Watu Pori Wilayani Ukerewe (Mwenye Fedha) akihesabu fedha zilizotolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa kama sehemu ya ahadi yake baada ya kuzindua shina hilo mwishoni mwa mwaka jana. Kulia ni Katibu Mkuu CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akizungumza baada ya kukabidhi fedha hizo.
Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Mwanza ikiwa katika Shule ya Msingi Lutare Wilayani Ukerewe ambapo kutokana na Shule hiyo kukabiliwa na dawati zipatazo 160, Katibu huo alitoa dawati 30 huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe nae akiongeza dawati nyingine 20 na hivyo kufanya jumla ya dawati 50 kupatikana katika ziara hiyo. Mtaturu alitoa rai kwa wadau wengine wa elimu kujitokeza kusaidia utatuzi wa changamoto ya upungufu wa dawati katika shule hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akisalimiana na Wana-CCM wajao katika kijiji cha Chabilungo kilipo chanzo cha maji cha mradi wa maji vijijini unaotekelezwa Wilayani Ukerewe.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti wakizungumza na baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Soka ya Kijiji cha Chabilungo ambapo kuna chanzo cha maji cha mradi wa maji vijijini katika Wilaya ya Ukerewe. Mtaturu alitoa fedha kwa ajili ya timu hiyo kununua mpira wa Miguu huku Mkirikiti akichangia jezi kwa ajili ya timu hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akipandisha bendera ya CCM baada ya kuzindua Shina la Wakereketwa wa CCM Stand Mpya ya Nansio.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nakatunguru Wilayani Ukerewe ambapo aliridhishwa na Ujenzi huo unavyoendelea.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Alietangulia) ikiendelea Wilayani Ukerewe.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mifuko ya Theluji 100 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara ya Shule za Sekondari Ilugwa pamoja na Nakoza iliyotolewa na Antony Diallo ambae ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza 
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akiwa katika Shina la Wakereketwa wa CCM Watu Pori.
Must Read
Must Read
Must Read
Akina mama Wilayani Ukerewe wakitoka kuhemea maji ziwa Victoria kutokana na bomba za maji Mjini Nansi Ukerewe kutotoa maji.
Vijana Wilayani Ukerewe wakiwa katika harakati za Kusearch Maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na biashara ambapo kwa sasa torori moja linauzwa kati ya shilingi elfu moja hadi shilingi elfu tatu kulingana na umbali.
SOURCE:METRO FM

No comments:

Powered by Blogger.