KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA AMTAKA MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARDHI WILAYANI HUMO.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatuturu akiwasili hii leo katika Ofisi za Chama hicho Wilaya ya Sengerema kwa ajili ya Ziara ya Siku mbili Wilayani humo.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza
kimemtaka Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Zainabu Telaki kushughulikia matatizo ya
ardhi, yanayowakabili wananchi wa Kijiji cha Mnadani Wilayani humo.
Katibu wa
Chama hicho Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatutu ametoa kauli hiyo hii leo katika
Viwanja vya CCM Wilayani Sengerema, wakati akiwahutubia wananchi katika Mkutano
wa hadhara.
Kauli ya
Mtaturu imejili kufuatia malalamiko kutoka kwa Wananchi wa Kijiji hicho,
kuwalalamikia maafisa wa ardhi Wilayani Sengerema kwa kushirikiana na
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnadani kuingia katika Mashamba yao kwa ajili ya
upimaji wa ardhi bila kushirikishwa.
Mtaturu
amebainisha kuwa sheria ya ardhi inaeleza wazi kuwa wananchi wanapaswa
kushirikishwa kwanza katika uendelezaji wa ardhi yao, hivyo kitendo cha
wananchi hao kutoshirikishwa katika upimaji wa ardhi yao ni uvunjifu wa sheria.
"Sheria ya ardhi iko wazi, kabla serikali haijaja kufanya chochote kwenye eneo lako lazima ikushirikishe...ukiona mtu anakuja kwako bila kukushirikisha mtoe nduki...wananchi hawa msiwaonee...Mkuu wa Wilaya shughulika na hii kitu...sisi shida yetu CCM wananchi matatizo yao yaishe" Amesema Mtaturu.
Awali akitoa
malalamiko yake kwa niaba ya Wananchi wengine, Imelda Mpanduji ambae ni
mwananchi wa Kitongoji cha Mnadani Wilayani Sengerema, amesema kuwa wananchi
wamechoka kuburuzwa na viongozi hao ambao wamekuwa wakiingia katika mashamba
yao na kupima ardhiri kinyemela na hivyo kumuomba katibu huo wa CCM Mkoa wa
Mwanza kuingilia kati suala hilo kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi.
Akijibu
Malalamiko ya Wananchi hao, Staimili Alexander Ndaro ambae ni Kaimu Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ameeleza kuwa viwanja vinavyolalamikiwa
na wananchi hao ni vile vinavyopitiwa na mradi wa kuendeleza Makazi ya wananchi
katika eneo hilo la Mnadani Wilayani Sengerema, hivyo kama kuna mwananchi ambae
amekosa kiwanja katika eneo hilo na ardhi yake imechukuliwa kwa ajili ya
matumizi mengine ya Umma, anapaswa kufika katika Ofisi za Halmashauri hiyo kwa
ajili ya kupatiwa kiwanja kingine.
Katibu wa
CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu ameanza ziara yake ya siku mbili Wilayani
Sengerema hii leo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika Wilaya za Mkoa wa
Mwanza ambapo pamoja na mambo mengine amekutana na Kamati ya Siasa, Halmashauri
kuu ya CCM ya Wilaya pamoja na kuzungumza na Wananchi katika Mkutano wa
hadhara.
Akiwa katika
kikao cha Halmashauri kuu ya CCM ya Wilaya ya Sengerema Mtaturu amewataka
wanachama wa chama wa chama hicho kuwa wamoja na kuachana na mgawanyiko ndani
ya chama ambapo ametahadharisha kuwa CCM bado iko imara na itaendelea kutawala
milele na milele.
Kesho ziara
hiyo inatarajiwa kuhitimishwa ambapo Mtaturu anatarajia kukagua shughuli za
miradi ya maendeleo ambazo ni pamoja na kukagua miradi ya maji Luchili, Lumeya,
Nyakaliro lakini pia kukagua Maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Isaka Nyehunge
na hatimae kutamatisha ziara hiyo kwa kufanya Mkutano wa hadhara katika Kijiji
cha Nyakaliro Jimboni Buchosa.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Aliesimama) akizungumza na Halmashauri ya CCM Wilaya ya Sengerema hii leo.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Zainabu Telaki (aliesimama) akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Serikali ya Mwaka 2010/15 katika kikao cha halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Sengerema kilichofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Sengerema.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Sengerema wakiwa katika kikao na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Alie Jukwaani) akiwahutubiwa wananchi Wilayani Sengerema katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya CCM Wilayani humo.
Wananchi na Wanachama wa CCM wakimsikiliza Katibu wa ccm Mkoa wa Mwanza.
Watendaji pamoja na Viongozi wa CCM na Serikali Wilayani Sengerema.
Watendaji pamoja na Viongozi wa CCM na Serikali Wilayani Sengerema.
Akijibu Malalamiko ya Wananchi hao, Staimili Alexander Ndaro ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema akijibu malalamiko ya Wananchi kuhusiana na upimaji wa ardhi yao bila kushirikishwa.
SOURCE:99.4 METRO FM
No comments: