LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA NI NOMA. TAMAZA ZIARA ZAKE KATIKA WILAYA YA SENGEREMA.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye Miwani) akiwasili katika Uwanja wa Nyakaliro Wilayani Sengerema kwa ajili ya Mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja hivyo. Katibu huo amehitimisha ziara yake ya Siku mbili Wilayani Sengerema ambapo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya maji, hospitali pamoja na kukutana na viongozi mbalimbali wa chama.

Kesho jumamosi Mtaturu anatarajia kufanya ziara ya siku mbili katika Wilaya ya Misungwi ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake alizozianza March 23 katika Wilaya ya Ukerewe na kufuatiwa na Wilaya ya Sengerema ambapo lengo ni kutembelea Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wananchi pamoja na wanachama wa CCM pamoja na kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010/15.
Na:George Binagi-GB Pazzo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akisalimiana na Wananchi wa Jimbo la Busega Wilayani Sengerema baada ya kuwasili Jimboni humo kwa ajili ya Mkutano wa hadara uliofanyika katika Uwanja wa Nyakaliro na kukusanya wananchi wengi kutoka vyama mbalimbali vya siasa.
Wananchi wakimsikiliza Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu wakati akihutubia hii leo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Nyakaliro Jimbo la Busega Wilayani Sengerema.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa akimwaga Sera katika Mkutano wa hadhara uliofanyika hii leo katika Uwanja wa Nyakaliro ambapo Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alikuwa akihutubiwa wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema ambae pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba (CCM) akitoa salamu zake kwa wapiga kura wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Nyakaliro Jimbo la Buchosa ambapo Katibu wa ccm Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alikuwa akihutubia ikiwa ni katika kuhitimisha ziara yake ya siku mbili wilayani Sengerema hii leo.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema ambae pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba (katikati alieweka mkono mfukoni) akiwa katika Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Wa kwanza Kushoto) akimsikiliza mtalaamu anaejenga mashine ya kusukuma maji kutoka katika chanzo cha maji cha Lumeya katika Jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye Miwani) akipokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Maji katika chanzo cha Maji Nyamazugo Wilayani Sengerema.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye Miwani) akikagua mashine ya kusukuma maji kutoka katika chanzo cha Maji Lumeya katika Jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema. Miraji amemtaka PET Co-operation ambae ni mkandarasi anaetekeleza mradi huo kuhakikisha kwamba hadi kufikia April 22 mashine hiyo iwe imeanz kufanya kazi kwa ajili ya wananchi wa Sengerema kupata huduma ya maji safi na salama.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu ikikagua jengo la Utawala la Hospitali ya Isaka iliyopo Nyehunge katika Jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema. Hadi kukamilika kwake mradi huu utagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 24.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akiwa na Leah James (Katikati) ambae ni Balozi wa CCM shina namba Sita katika Mtaa wa Barabara ya Geita Wilayani Sengerema ambapo kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sengerema Chasama Kamata. Mtaturu amemtembelea balozi huyo hii leo wakati akiwa katika ziara ya siku mbili ambayo imehitimishwa hii leo Wilayani Sengerema.
Wajumbe wa Balozi wa Shina namba Sita Mtaa wa Barabara ya Geita Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wakiimba wimbo wa Kumkaribisha Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu mara baada ya kuwatembelea hii leo akiwa katika ziara ya siku mbili Wikayani Sengerema. Ziara hiyo ilianza jana na imehitimishwa hii leo.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Sengerema wakiwa pamoja na viongozi wa chama hicho Mkoa wa Mwanza akiwemo Katibu wa Chama hicho Miraji Mtaturu (Mwenye Miwani) wakiimba wimbo wa Chama mara baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Nyakaliro Jimbo la Buchosa kwa ajili ya Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu huo wa CCM Mkoa wa Mwanza.
CHANZO: METRO FM

No comments:

Powered by Blogger.