LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI WA SAMAKI. TAZAMA KUPITIA BINAGI TV.

Na:George GB Pazzo
Wananchi na Wakazi wote wa Kanda ya Ziwa wamehamasishwa kuhudhuria Mafunzo ya Ufugaji wa Samaki Kibiashara yanayotarajiwa kufanyika Wiki hii katika Ukumbi wa Midland Hotel Jijini Mwanza.

Wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo, JKT Buramba Bunda, Japani pamoja na Ujerumani wanatarajiwa kuwepo kwa ajili ya kutoa elimu ya mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Kampuni inayowawezesha wajasiriamali mbalimbali hapa nchini ya PSP Mwezeshaji Concultancy.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa Kesho Alhamisi ya April 16 Midland Hotel kuanzia saa 06:00 za Jioni hadi saa 08:00 za Usiku kwa gharama ya Shilingi 65,000 ikiwa ni gharama ya mafunzo pamoja na chakula cha usiku.

Mkurugenzi wa PSP Mwezeshaji Concultancy Protase Semuhomyi amewasihi wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya Mafunzo ya Ufugaji wa Samaki Kibiashara kwa lengo la Kujikomboa kiuchumi hususani katika kipindi hiki ambacho Taifa linakabiliwa na uhaba wa ajira.

Ili kuthibitisha Ushiriki wako katika Mafunzo hayo, wasiliana na Waandaaji wake kwa nambari +255 784 690 712, +255 753 778 571, au +255 766 09 41 10. 
                                          TAZAMA TANGAZO KUPITIA BINAGI TV HAPA CHINI

CREDIT: PSP MWEZESHAJI CONSULTANCY

No comments:

Powered by Blogger.