LIVE STREAM ADS

Header Ads

HAWA NDIYO WATANGAZAJI NA MADJZ WAPYA WALIOJIUNGA NA RADIO METRO FM YA JIJINI MWANZA.

Baada ya Mchujo mrefu wa Kuwapata Watangazaji wapya kwa ajili ya Kujiunga na Team ya 99.4 Radio Metro Fm ya Jijini Mwanza, hatimae Watangazaji Saba na Dj Mmoja wameweza kupenya vigingi kibao na hatimae kujiunga na Radio hiyo ambayo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011 imekuwa Radio Pendwa zaidi kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa katika masuala ya Habari, Burudani na Matangazo.
Na: George GB Pazzo
Katika Picha hapo juu ni miongoni mwa Watangazaji waliofanikiwa kujiunga na 99.4 Radio Metro ambapo kutoka kushoto na kipindi anachosikika ni Hezekiah Francis (Afro Cheers- Mindule ya Moto), Barazeduka Anselmo (Mambo Mtelezo), Genya Richard (Michezo leo na Segments zote za Michezo na Zilipendwa-Muziki wa Zamani), Alex Gwido (Pambazuko la Metro Fm) pamoja na Sophia George (Mambo Mtelezo). Wengine wawili ambao hawako pichani ni Jay Joh (Jam Session) pamoja na Katumba Madua (Pambazuko la Metro Fm na Zilipendwa).

Mchakato wa Kuwapata Maproducers bado unaendelea ambapo Waliopita katika Mchujo wa kwanza bado wanaendelea kumenyana kwa kutengeneza kazi zao ili waweze kupatikana watakaokuwa the best ambapo kwa Upande wa MaDjz tayari Dj God (hayuko pichani) amekwisha jiunga na Team ya Metro Fm na anasikika katika Kipindi cha Jam Session.
Watangazaji wapya waliojiunga na Radio Metro Fm ya Jijini Mwanza na vipindi wanavyosikika katika mabano ambapo kutoka kushoto ni Hezekiah Francis (Afro Cheers-Mindule ya Moto), Barazeduka Anselmo (Mambo Mtelezo), Alex Gwido (Pambazuko la Metro Fm), Sophia George (Mambo Mtelezo) pamoja na Richard Genya (Michezo leo na Segments zote za Michezo na Kipindi cha Zilipendwa-Muziki wa Zamani).
Kushoto ni Host wa Kipindi cha Mambo Mtelezo cha Metro Fm Amina Rashidi (Yeye ni Mkongwe) akiwa pamoja na Sophia George (Katikati) akifuatiwa na Barazeduka Anselmo (Kulia).
Mtangazaji Mpya wa Kipindi cha Jam Session Jay Joh (Kushoto) akiwa pamoja na Dj wa Kipindi hicho Dj God (Kulia) ambae pia ni Dj Mpya Metro Fm.
Mmoja wa Watangazaji wapya wa Metro Fm Katumba Maduwa a.k.a Mc.Katumba Mzee wa Viumbe hai (Wanyama pamoja na Ndege) ambae anasikika kupitia kipichi cha Pambazuko la Metro Fm pamoja na Zilipendwa-Muziki wa Zamani.
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTION

1 comment:

  1. Nijambo jema kuwa na media nyingi nchi hii ni kuonyesha uhuru wa vyombo vya habari umekomaaa Tanzania, lakini je watangazaji wapya wanafuata maadili kama ya zamani. Hongereni METRO FM KWA KUPATA WATANGAZAJI WAPYA, ILA TUNAOMBA MUONGEZE URUSHAJI WA MATANGAZO YENU, KWANI SI KANDA YA ZIWA YOTE MNAPATIKANA KAMA MNAVYO JITANGAZA. MUSOMA MJINI HAMPATIKANI NA TUNA HAMU KUBWA XANA YA KUTAKA KUWASIKIA KWA UJIO WENU KATIKA KANDA YA SAMAKI( KANDA YA ZIWA)

    ReplyDelete

Powered by Blogger.