HATUA ZAANZA KUCHUKULIWA ILI KUONDOA HATARI YA MAGONJWA YA MINYOO NA KICHOCHO MWANZA.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu).
Na:Elisa Anatory
Imeelezwa kuwa Mkoa wa Mwanza unaongoza
kwa kuwa na wagonjwa wengi wa minyoo ya
tumbo pamoja na ugonjwa wa kichocho ambao
husababisha saratani ya kibofu cha
mkojo.
Hayo yalisemwa ijumaa iliyopita na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka
Konisaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, wakati akizungumza katika kikao
cha kuratibu kampeni ya chanjo ya kuzuia magonjwa ambayo yamekuwa hayapewi
kipaumbele inayotarajiwa kutolewa bure Mkoani Mwanza wiki hii.
Aliyataja magonjwa hayo kuwa ni pamoja na ugonjwa wa kichocho, minyoo ya tumbo pamoja na trakoma ambapo alisema
kuwa utafiti uliyofanyika mwaka 2005 ulionesha kuwa maabukizi ya Magonjwa hayo Mkoani Mwanza ni kati ya asilimia 12.7 hadi asilimia 87.6 na hivyo kufanya
Mkoa huo kuongoza kwa maambukizi ya Magonjwa hayo nchini.
Aidha Konisaga aliongeza kuwa ugonjwa huo umeenea kwenye maeneo
yote yanayozunguka ziwa Viktoria ambapo aliongeza kuwa Mkoa wa Mwanza
utaendelea na kampeni ya ugawaji wa dawa za kukinga na kutibu magonjwa hayo bure
kabisa kuanzia tarehe 26 hadi 27 mwezi huu katika Wilaya zote ambapo walengwa
wa kampeni hiyo ni watoto wote wenye umri wa kuanza darasa la kwanza.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu hospitali ya Mkoa wa Mwanza
Sekour Toure James Kengia ambaye pia ndiye Mratibu wa kampeni hiyo alisema kuwa
zaidi ya watoto Laki Sita wanatarajiwa kupatiwa huduma hiyo ya chanjo ya Kuzuia
Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika Mkoa wa Mwanza.
No comments: