SERIKALI KUWAREJESHA WAHAMIAJI HARAMU MAKWAO.
Serikali inatarajia
kuwarejesha kwao jumla ya waamiaji
haramu 91 raia wa Ethiopia,
walioingia nchini kinyume cha sheria ambao wamemaliza adhabu ya kutumikia
vifungo vyao.
Hayo yalisemwa hii leo bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa maMambo ya Ndani ya nchi Pereira Silima, alipokuwa akijibu swali
la Amina Kremensi mbunge wa Koani aliyetaka kujua mikakati ya serikali juu ya
waamiaji haramu nchini.
Waziri Silima aliongeza kuwa
hadi sasa jumla ya waamiaji 250 kutoka Ethiopia wamekematwa katika mikoa
mbalimbali nchini, ikiwemo Mbeya, Tanga, Mwanza pamoja na Mara ambapo 91 kati ya waliokamatwa kutumikia vifungo walivyopewa na hivyo Serikali inatarajia kuwarudishwa nchini kwao.
Aidha waziri Silima aliongeza kuwa serikali
inachukua hatua mbalimbali za kupambana na waamiaji haramu wanaoingia nchini
ikiwemo kuimalisha ulinzi katika mipaka yote pamoja na kuwafikisha mahakamani wale wanaokamatwa kwa kuingia nchini bila kibali.
Alibainisha kuwa wizara yake inatarajia kutoa elimu kwa viongozi na watu wote wanaoishi katika maeneo
ya mipakani ili kuweza kuwatambua wahamiaji na kutoa taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama.
No comments: