CHEMBA YA WAFANYABIASHARA WENYE VIWANDA NA KILIMO TCCIA YAIOMBA SERIKALI KUONDOA VIKWAZO VYA KIBIASHARA.
Picha ya Pamoja
Na:George GB Pazzo
Serikali imeombwa kuendelea kutatua Vikwazo
mbalimbali katika Sekta ya biashara nchini, kwa lengo la kuimarisha sekta hiyo
kwa wafanyabiashara ndani na nje ya nchi.
Ombi hilo lilitolewa mapema hii leo Jijini
Mwanza na Peter Chisawillo ambae ni Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini TCCIA nchini, katika semna ya Wafanyabiashara na Wadau
mbalimbali wa biashara kutoka Sekta binafsi na Serikali.
Chisawillo alisema kuwa bado kuna
baadhi ya vikwazo ambavyo vinahitajika kutatuliwa, kwa lengo la kusaidia ukuaji
wa Sekta ya biashara nchini jambo ambalo pia litasaidia katika ukuaji wa Uchumi
nchini.
Alivitaja baadhi ya Vikwazo hivyo kuwa
ni pamoja na upotevu wa Muda kutokana na bidhaa kuchukua muda mrefu katika
maeneo ya mizani pamoja na kuondoa usumbufu maeneo ya mipakani wakati wa
ukaguzi wa bidhaa zinazoingia ama kutoka nchini.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza
Elibariki Mmari aliomba kuondolewa kwa vikwazo katika maeneo ya Mipakani
pamoja na Vizuizi vya barabarani ambapo ameobainisha kuwa bado kuna vikwazo vingi vinavyokwamisha biashara katika maeneo hayo licha ya kuwepo kwa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza, Ndaro Kulwijira ambae ni Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza alisema kuwa
Serikali itaendelea kupunguza changamoto na vikwazo mbalimbali ambavyo
vinaivyoikabili Sekta ya biashara nchini ambapo amebainisha kuwa ili
kufanikisha suala hilo, Sekta ya Biashara imeingizwa katika Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa BRN.
Semna hiyo ya Wafanyabiashara imelenga
kujadili Changamoto na Vikwazo mbalimbali vinazowakabili Wafanyabiashara nchini
na namna ya kuvikabili huku ikitarajiwa kufikia tamati Ijumaa wiki hii ambapo
kutakuwa na Mkutano Mkuu wa TCCIA.
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndaro Kulwijira ambae alimwakilia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika Semina ya Wafanyabiashara kutoka TCCIA iliyoanza hii leo Jijini Mwanza akizungumza na Wanahabari.
Peter Chisawillo ambae ni Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo nchini TCCIA nchi akizungumza na Wanahabari
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza Elibariki Mmari
Washiriki wa Semna
Semna ikiendelea kutolewa
Sekretarieti ya TCCIA
Washiki wa Semna
Semna imewashirikisha Viongozi wa TCCIA nchini ambao ni pamoja na Wenyeviti, Makatibu pamoja na Wajumbe.
No comments: