LIVE STREAM ADS

Header Ads

KIRUMBA BOYS YAISHIKISHA ADABU SEVILLA FC KATIKA MICHUANO YA SOKA YA RAMADHAN CUP.

Na:Osicar Mihayo
Mashindano ya mfungo Mtukufu wa Ramadhani (Ramadhan Cup) yanayofanyika katika Uwanja cha Magomeni Kirumba yamezidi kushika kasi ambapo timu ya soka ya Kirumba Boys imeikung'uta mabao 3-1 timu ya Sevilla Fc zote kutoka Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.

Wafungaji wa mabao ya Kirumba Boys katika mpambano huo uliochezwa juzi walikuwa ni Benjamin Ojolomongo, Nguzumari Elisha na Zabron Kanoni , huku bao la kufutia machozi la Sevilla Fm likifungwa na Yassin Twahibu katika kipindi cha kwanza.

Mashindano hayo yamelenga kuwatoa vijana kutoka katika makundi maovu katika kipindi hiki cha mfungo huu mtukufu wa Ramadhani yanatarajia kuendele hapo kesho ambapo kutakuwa na mchezo kati ya Gold Sports dhidi ya Kabuhoro Fc ambapo mshindi atacheza na Kirumba boys ngazi ya Mtoano.

Kocha wa Kirumba Musa Pius alisema kuwa siri ya ushindi huo ni kujituma kwa wachezaji wake kwani hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, walikuwa nyuma kwa bao moja lakini kipidi cha pili wachezaji wake walizinduka kutoka usingizini na kusawazisha kwenye dakika ya 56 ya mchezo kabla ya kuongeza bao la pili na la tatu katika dakika ya 82 ya mchezo huo.

Pius alitoa wito kwa vijana wapenda michezo kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono kwani kufanya hivyo ndiyo itakuwa nguzo yao muhimu ya wao kuchukua kombe hilo la Ramadhan Cup ambalo linashirikisha Timu za daraja la nne kutoka Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.