LIVE STREAM ADS

Header Ads

KISHIMBA AWAOMBA RADHI WANAKAHAMA KWA KUWATELEKEZA KWA MUDA WA MIAKA 15.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (Kulia) akipokea mchango wa shilingi milioni 15 kutoka kwa Mfanyabiashara wa Mwanza na Dar es salaam Jumanne Kishimba (Kushoto) katika harambee ya kuchangia  Mradi wa Mkapa Fellows iliyofanyiak kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza mwaka jana.
Na:Shaban Njia
Mtia nia ya kugombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo jipya la Kahama Mjini Jumanne Kishimba juzi aliwaomba radhi wananchi wa Kahama kwa kutokugombea kiti hicho kwa muda wa miaka 15 iliyopita.

Kishimba aliomba radhi hiyo wakati akiongea na Mtandao huu ambapo alibainisha kuwa ameamua kuacha biashara zake pembeni ili kugombea Ubunge katika jimbo jipya la Kahama Mjini katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kuwa ni muda mrefu amewatekeleza Wananchi wake alipokuwa akijihusisha zaidi na biashara..

Alisema kuwa sio kwamba ameacha biashara zake bali ameamua kurudi katika ulingo wa siasa kwa lengo la kuwaletea wana Kahama mabadiliko hasa katika Nyanja za uchumi na biashara ambazo amekuwa ni mzoefu wa miaka mingi katika masuala hayo.

Pia Aliendelea kusema kuwa tangu aache kugombea Ubunge kwa muda wa miaka 15 sasa kumekuwa na changamoto nyingi katika Wilaya ya Kahama kwa ujumla hasa katika sekta mbalimbali ikiwemo uchumi.

“Kahama ni moja ya Wilaya zinazokuwa kiuchumi kwa kasi hapa nchini, kwa kutumia uzoefu wangu wa kufanya biashara hasa zile za kimataifa ninaweza kuwasaidia wafanyabiashara wa kahama katika kupata fursa za kufanya biashara kubwa na za kimataifa ili kuinua mitaji yao”, Alisema Kishimba.

Pamoja na Mambo mengine muonesha nia huyo huyo alisema kama CCM itampatia ridhaa ya kupeperusha bendera katika kugombea kiti hicho kahama Mjini atahakikisha anajitahidi katika kuhakikisha kuwa Wilaya ya Kahama inakuwa na kupiga hatua katika sekta za Afya, Maji pamoja na Elimu.

“Ili uweze kupata mafanikio katika maisha lazima watu wasome kwa bidii ili kupata wasomi wengi hali ambayo itasaidia kukuza maendeleo kama mimi nilivyoamua kujenga Shule ya Sekondari ya Kishimba na kuikabidhi serikali hali hii inapaswa kuigwa na watanzania wengi”, Aliongeza Jumanne Kishimba.

Alisaema kuwa kwa kutumia uzoefu wake alionao katika biashara za kimataifa Kishimba alisema kuwa ataweza kujenga ushawishi kwa kuwainua Wafanyabiashara wadogo waone umuhimu wa kuwekeza katika Elimu ili kuweza kuifanya Wilaya ya Kahama kuwa hata na chuo kikuu kimoja kutokana na kupanda kwa hadhi yake na kuwa Manispaa kwa sasa.

Katika kinyanganyiro hicho cha kugombea Ubunge kwa Jimbo la Kahama Mjini kuna jumla ya Wagombea 14 ambao tayari wameonyesha nia ya kulitaka Jimbo hilo jipya kwa tiketi ya Chama hicho hali ambayo imeleta ushindani mkubwa baina ya Wagombea hao.
Powered by Blogger.