LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA MKOANI MWANZA. MKUU WA MKOA ATOA ONYO KALI KWA WANAOHATARISHA AMANI.

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kamandi ya Mwanza wakipiga risasi angani ishara ya kuwakumbuka mashujaa wa Tanzania waliopoteza maisha katika vita za ukombozi wa Tanzania.

 Ilikuwa hii leo katika Mnara wa Mashujaa Jijini Mwanza uliopo katika Mzunguko wa barabara za Kenyatta, Makongoro na Nyerere yalipofanyika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Mkoani Mwanza ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Stanslaus Mulongo.
 Picha zote na Atrey Kuni; Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza

Imeandikwa na:George GB Pazzo
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Stanslaus Mulongo amesema kuwa kamwe hatavumilia kuona Amani na Usalama wa Mkoa wa Mwanza vinatoweka, kutokana na baadhi ya watu hususani katika kipindi cha kuelekea katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.

Mulongo ametoa kauli hiyo hii leo wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa nchini, ambayo katika Mkoa wa Mwanza yamefanyika katika Mnara wa Mashujaa uliopo katika mzunguko wa barabara ya Nyerere, Makongoro na Kenyatta Jijini Mwanza ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Leo hii tunawakumbuka mashukaa wetu waliopoteza maisha katika kupigania ukombozi wa Taifa letu. Ni siku ambayo inatukumbusha juu ya kutunza amani ambayo mimi na wewe tunawajibu wa kuilinda kwa misingi ya uzalendo maana vita siyo nzuri".Alisema Mulongo nakuongeza;

"Wanaolimbea taifa vita washindwe na walegee maana kuna baadhi ya watu hususani viongozi wa kisiasa wameanza kuhubiri  masuala ya kuvuruga amani, sasa mimi niwaambie hapa si pahala pa kuchezea hivyo niwaombe sana hata tunapoelekea katika uchaguzi mkuu, kila mchakato unaopita, upite salama maana kama kuna mtu anajiandaa kuvuruga amani ya mkoa huu cha moto atakiona". Alitanabaisha Mulongo.

Aidha Mulongo amesema kuwa Mwanza siyo pahali pa kuchezea hivyo hatavumilia kuona wanasiasa wanaendesha siasa zisizo za kistaarabu ambapo amewatahadharisha kufanya mikutano yao kwa kufuata taratibu ambapo amekemea maandamano na mikutano isiyo na kibali.

"Niviombe Vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Mwanza kusimamia vyema majukumu yake na hatutaki askari legelege ambao hawatatimiza majukumu yao vyema". Alisema Mlongo.

Wakati maadhimisho hayo Siku ya Mashujaa yakifanyika, bado baadhi ya mashujaa walioshiriki katika vita mbalimbali za ukombozi nchini wanalalamika kusahaulika katika kupatiwa stahiki zao na serikali.

"Serikali bado haitukumbuki. Wapo ambao walipata mafao kidogo lakini wapo ambao walisahaulika na hii Serikali yetu licha ya kwamba sisi ndiyo tuliolipigania Taifa hili". Anasema Mzee Ibrahim Sadal (90) ambae alikuwa mpiganaji katika Jeshi la Tanganyika enzi hizo likijulikana kama Kings African Rifles (KAR) ambapo alipigana vita ya pili ya dunia tangu mwaka 1939 hadi mwaka 1945. 

Siku ya Majushaa nchini huazimishwa Julai 25 kila mwaka ikiwa ni tarehe ambayo mashujaa waliopigana vita ya Kagera walirejea nchini wakiotokea Uganda, ikiwa imelenga kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha katika vita hiyo ambapo Kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam, mgeni rasmi akiwa ni rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kamandi ya Mwanza wakiwakumbuka mashujaa wa Tanzania waliopoteza maisha katika vita za ukombozi wa Tanzania.
Waliokaa kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, Kanari wa Jeshi la Wananchi Kamandi ya Mwanza Kanari Kivambi pamoja na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndaro Kulwijira.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akijiandaa kuweka Mkuki na Ngao katika Mnara wa Mashujaa Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akiweka Mkuki na Ngao katika Mnara wa Mashujaa Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akiongea katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akiongea katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Mkoani Mwanza.
Askofu wa Kanisa la CPTC Zebedius Isaya akiweka Shada la Maua katika Mnara wa Mashujaa Mkoani Mwanza.
Sheikh Ibrahim akiweka Shada la Maua katika Mnara wa Mashujaa Mkoani Mwanza kwa niaba ya Sheikh Mkuu wa Mkoa.
Sheikh Ibrahim Mauba akiomba dua katika siku ya Mashujaa Mkoani Mwanza kwa niaba ya Sheikh Mkuu wa Mkoa.
Mtumishi Paulo Mashiba akiwaombea Mashujaa kwa niaba ya Askofu wa Kanisa Katholic Jimbo la Mwanza.
Askofu wa Kanisa la CPTC Zebedius Isaya akiomba dua katika Mnara wa Mashujaa Mkoani Mwanza.
Mzee Ibrahim Sadal (90) ambae alikuwa mpiganaji katika Jeshi la Tanganyika enzi hizo likijulikana kama Kings African Rifles (KAR) ambapo alipigana vita ya pili ya dunia tangu mwaka 1939 hadi mwaka 1945 akiweka sha la maua katika mnara wa mashujaa Mkoani Mwanza. 
Kutoka Kushoto ni Askofu wa Kanisa la CPTC Zebedius Isaya, Mtumishi Paulo Mashiba wa kanisa Catholic Jimbo la Mwanza, Sheikh Ibrahim Mauba pamoja na Mzee Ibrahim Sadal (90) ambae alikuwa mpiganaji katika Jeshi la Tanganyika enzi hizo likijulikana kama Kings African Rifles (KAR) ambapo alipigana vita ya pili ya dunia tangu mwaka 1939 hadi mwaka 1945.
Viongozi mbalimbali wa dini, Seikali na Jeshi.
Viongozi mbalimbali wa dini, Seikali na Jeshi.
BINAGI MEDIA GROUP TUNASEMA TUIDUMISHE AMANI YA TAIFA LETU, WAKATI TUNAWAKUMBUKA MASHUJAA WETU KWANI VITA SI MCHEZO WA KIRAFIKI.
Powered by Blogger.