LIVE STREAM ADS

Header Ads

ASKOFU WA KANISA KATOLIKI JIMBO LA KAHAMA AHOFIA KANISA HILO KUKOSA MAPADRI.

Na:Shaban Njia
Askofu wa kanisa Katoliki jimbo la kahama Ludovick Minde amewataka wazazi na walezi kuwalea watoto wao katika misingi ya kulipenda kanisa na kuwapeleka katika shule za kichungaji ili waweze kuwa watawa na mapadri jambo litakalosaidia kanisa hilo kuendelea kuwa na viongozi wadilifu.

Aliitoa kauli hiyo jana ikiwa ni muda mfupi baada ya kuwawekea mikono ya daraja la upadri waliokuwa mashemasi wa kanisa hilo ambao ni Padri Jastine Bahati kutoka parokia ya Mbogwe na padri Endrew Henry Lupondya kutoka parokia ya Nyasubi mjini Kahama.


"Watoto wengi wamekuwa na doto za kuwa  watumishi wa mungu lakini ndoto hizo zimekuwa zikiyeyuka kutokana na malezi duni ya wazazi ama walezi wao ambao hawataki kuwalea katika misingi ya kumutumikia mungu na hivyo kusababisha kanisa kuwa katika hatari ya kuwakosa mapadri". Alisema askofu Minde.


Hata hivyo amewataka mapadri ambao wamepadirishwa kuhakikisha kuwa wanafanya kazi ya kanisa ili kuliendeleza taifa la Mungu na kuwataka kuwatendee mema watu na wasichoke kulihubiri neno la Mungu popote pale duniani.


Wakitoa shukrani zao kwa baba askofu, mapadri hao wateule walisema kuwa haikuwa kazi rahisi kufikia  daraja la Upadri walilofikia ambapo walibainisha kuwa mwenyezi Mungu ndiye alisaidia katika kufikia hatua hiyo.

Walisema kuwa wanawashukuru wazazi  wao wa kimwili na wazazi wa kiroho kwa kuendelea kuwatia moyo katika safari yao ya utume na kwamba wamejiandaa vyema kumutumikia Mungu kwa kuchunga kondoo wake.

"Kazi ya utume inahitaji maombi ya kila mwamini na ili tuweze kuitimiliza vyema tunahitaji msaada wa waumini na viongozi wetu ambao walitutangulia jambo litakalotuwezesha kuifanya na kuitimiliza vyema kazi kuchunga kondoo wa bwana iliyo mbele yetu". Walitanabaisha Mapadiri hao.

No comments:

Powered by Blogger.