LIVE STREAM ADS

Header Ads

BAADA YA KUPOKELEWA KISHUJAA NA WANAKAHAMA, LEMBELI AITAHADHARISHA CCM.

Mh.James Lembeli
Na:Shaban Njia
Aliekuwa mbunge wa Jimbo la Kahama James Lembeli amesema kuwa kitendo chama cha Mapinduzi (CCM) kama kitamteua Jumanne Kishimba kugombea Ubunge katika jimbo jipya la Kahama mjini atamdhalilisha vibaya katika uchaguzi huo.

Lembeli ambaeye hivi karibuni amekihama chama cha Mapinduzi na kujiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) alisema kuwa kama CCM itampa ridhaa Jumanne Kishimba kugombea Ubunge katika Jimbo hilo atakuwa amedhalilishwa kwa kuwa mgombea huyo hatoshi kwake.

Akihutubia mamia ya wanakahama kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika viwanja vya CDT mjini Kahama, Lembeli alitanabaisha kuwa yeye ni miongoni mwa watia nia wa kugombea ubunge jimbo la Kahama mjini kwa tiketi ya CHADEMA na kwamba kama kura kumpitisha kugombea hazitatosha hatakuwa na tatizo lolote juu ya matokeo atakayoyapata.

“Najua kuondoka kwangu CCM kutawaumiza wengi na wasinisikitikie mimi bali wawasikitikie viongozi wao waliosababisha mimi nihamie chama kingine.” Alisema Lembeli.

Akiongelea kumshambulia Jumanne Kishimba kwa maneno makali  Lembeli alimtaka mgombea huyo kuhakikisha kuwa  anajitoa katika kinyang’anyiro hicho ili kulinda heshima yake kwani naye ni mtoto wa chifu kama alivyo yeye.

Lembeli pia aliwahakikishia viongozi wa CHADEMA kuwa  atahakikisha majimbo yote ya Mkoa wa Shinyanga  yanarejea CHADEMA  na kuvunja ngome zote za chama cha Mapinduzi zilizopo katika Mkoa huo.

Lembeli alisema pamoja na kuliongoza jimbo hilo katika kipindi cha miaka kumi  lakini chama hicho hakijaona umuhimu wa kuthamini mchango wake katika kuleta maendeleoya kwa wananchi wa jimbo la Kahama.

Lembeli aliyeingia kwa staili ya kubebwa na wananchi kama chifu alitokwa na machozi kwa kutotegemea kukuta umati mkubwa wa wakazi wa Kahama waliojitokeza kumpokea katika viwanja hivyo huku akiongozana na mama yake mzazi (mwana Maria).

“Machozi haya yasitabiriwe  vibaya kwani haijawahi kutokea umati mkubwa kama huu wa watu kujitokeza kwa ajili yangu tangu nianze kazi ya Ubunge katika jimbo hili la Kahama, Niliwahi kuwaleta viogozi wakubwa wa serikali hapa lakini umati kama huu haukujitokeza hivyo kwangu hii ni ajabu na sasa najiona kama nimeokoka”. Alisema Lembeli.

Katika  mkutano huo ambao Lembeli aliambatana na wabunge kutoka kanda ya ziwa akiwamo mbunge wa Nyamagana  Ezekiel Wenje, Mbunge wa Biharamulo Antony Mbassa pamoja na Mbunge wa Ilemela Highness Kiwia, aliwataka pia wananchi wa Ushetu kufuata nyayo zake la sivyo itakula kwao.

Akiwasalimia wananchi wa Kahama, Mbunge wa jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje aliitupia lawama kwa serikali kuwatelekeza wakulima wa zaola Pamba na kusema kuwa ni bora wakauza miwa kuliko kulima zao hilo.

No comments:

Powered by Blogger.