VIONGOZI WA CHAMUITA KANDA YA ZIWA WATAMBULISHWA RASMI.
Viongozi wa CHAMUITA ambapo kutoka Kushoto ni Mjumbe Sospeter Tawo, Katibu Mwenezi Taifa Stella Joel, Katibu Mwenezi Kanda ya Ziwa Maganga James Gwensaga, Mkurugenzi wa Itifaki Taifa Magreth Sembuche, Katibu Mwanza Vanessa Laban, Mjumbe Taifa Ulimbaga Mwakatobe na Makamu Mwenyekiti Kanda ya Ziwa Emmanuel Mwakisepe wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwatambulisha viongozi wa chama hicho Kanda ya Ziwa jana.
Na:George GB Pazzo
Chama
cha Muziki wa Injili Tanzania CHAMUITA jana kimewatamulisha rasmi Viongozi wake
wa Kanda ya Ziwa, ambao watashirikiana na Waimbaji wa Muziki huo ili kuhakikisha
kuwa Waimbaji hao wananufaika na kazi
zao.
Kabla ya Viongozi hao kutambulishwa katika kikao
kilichofanyika Jijini Mwanza, Katibu Mwenezi wa Chama hicho Taifa Stella Joel
alisema kuwa lengo Kuu la Chama hicho ambacho kilianzishwa mwaka 2011 ni
kuwaweka wanamuziki wa Muziki wa Injili pamoja kwa ajili ya kutetea haki zao na
hatimae kunufaika na muziki wao.
“Lengo la Chama hiki cha Muziki wa Injili Tanzania
ni kuwaweka wanamuziki pamoja ili tuweze kuwa na sauti moja ya kutuwezesha kutetea
na kunufaika na kazi zetu, kama tunavyoona sasa hivi Muziki wa Injili unazidi
kukua na kuna pesa nyingi ambayo inapatikana lakini haiwafikii wanamuziki wa
injili". Alisema Joel na kuongeza;
"Kwa Mfano sasa hivi kuna kazi nyingi zinauzwa kwa njia ya mtandao kama
vile kuna Youtube, Miito ya Simu, Muziiki, Mkito na nyinginezo ambapo njia hizo
zinaingiza mabilioni ya pesa, na ndiyo maana tuliona kuna umuhimu wa kuanzisha
chama hiki kwa ajili ya kusimamia na kulinda haki zetu”. Alibainisha Joel ambae pia
ni mwimbaji wa Muziki huo wa injili.
Viongozi waliotambulishwa na chama hicho kwa
ajili ya Kusimamia shughuli zake Kanda ya Ziwa ni Mwenyekiti Emmy Lema, Makamu
Mwenyekiti Emmanuel Mwakisepe, Katibu Vanessa Laban, Katibu Mwenezi Maganga
Gwensaga pamoja na Mweka Hazina Sarah Gagala.
Akizungumza mara baada ya Utambulisho huo,
Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Kanda ya Ziwa Emanuel Mwakisepe, aliwahimiza wanamuziki wa
Muziki wa Injili kujiunga nacho kwa ajili ya kunufaika na manufaa yake ambayo
ni pamoja na kuwasaidizi kusajili wa nyimbo zao pamoja na chama kusimamia
taratibu za kufuata ili kunufaika na nyimbo zao pindi zinapokuwa zikitumika
katika mitandao mbalimbali ikiwemo miito ya simu na hata kuunganishwa na wasambazaji
wa muziki huo.
Nae Katibu Mwenezi wa CHAMUITA Kanda ya Ziwa
Maganga Gwensaga alisema kuwa chama hicho ndicho chama pekee ambacho kinatambulika
nchini kwa ajili ya kutetea haki na maslahi ya waimbaji wa muziki huo ambapo
alitanabaisha kwamba pia kinatambulika na Shirikisho la Vyama vya Muziki nchini
hivyo waimbaji wa Muziki huo wakitumie kwa ajili ya kufahamu masuala yao
mbalimbali ambayo yatawasaidia kunufaika na kazi zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Itifaki wa
CHAMUITA Taifa Magreth Sembuche aliwaomba wadau mbalimbali ambao ni pamoja na
wachungaji na wadhamini kujiunga na chama hicho kupitia uanachama wa heshima
lengo likiwa ni kukisaidia kufikia malengo yake ambayo ni pamoja na kuanzisha
redio kwa ajili ya kucheza muziki wa njili, lakini pia kufungua maduka katika
maeneo mbalimbali nchini yatakayokuwa yakiuza muziki huo jambo ambalo
litasaidia wanamuziki wa injili kunufaika na kazi zao zaidi.
Kwa wanamuziki wa Injili pamoja na Wadau
mbalimbali waliopo Kanda ya Ziwa ambao wanapenda kujiunga na CHAMUITA,
wanahimizwa kuwasiliana na Katibu Mwenezi ambae ni Maganga Gwensaga kwa nambari
+255 (0) 756 20 78 92 kwa ajili ya maelekezo na utaratibu zaidi.
Viongozi wa CHAMUITA ambapo kutoka Kushoto ni Mjumbe Sospeter Tawo, Katibu Mwenezi Taifa Stella Joel, Katibu Mwenezi Kanda ya Ziwa Maganga James Gwensaga, Mkurugenzi wa Itifaki Taifa Magreth Sembuche, Katibu Mwanza Vanessa Laban, Mjumbe Taifa Ulimbaga Mwakatobe na Makamu Mwenyekiti Kanda ya Ziwa Emmanuel Mwakisepe wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwatambulisha viongozi wa chama hicho Kanda ya Ziwa jana.
Kikao Kikiendelea
Majadiliano yakiendelea
Ni hoja juu ya Hoja kwa watumishi hawa wa Mungu kupitia Uimbaji
Kikao cha CHAMUITA Kanda ya Ziwa.
Kikao cha CHAMUITA Kanda ya Ziwa.
Kikao cha CHAMUITA Kanda ya Ziwa.
Kikao cha CHAMUITA Kanda ya Ziwa.
Kikao cha Chama cha Kuwatambulisha viongozi wa Muziki wa Injili Tanzania wanaowakilisha Kanda ya Ziwa kilifanyika jana Vinazo Hotel Jijini Mwanza.
No comments: