LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTATURU ASEMA MAGUFULI NDIYE RAIS WA TANZANIA MWAKA 2015 MAANA WAPINZANI HAWANA AJENDA.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akihutubia katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza.
 Na:George GB Pazzo
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu amesema kuwa mgombea Urais aliepitishwa na Chama hicho Dkt.John Pombe Magufuli, ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa anakubalika na watu wote nchini wakiwemo wapinzania.

Mtaturu alitoa kauli hiyo jana katika Mkutano wa hadhara wa Chama hicho, uliofanyika katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza ukiwa umelenga kuimarisha uhai wa chama.

"Magufuli ndiye Rais wa Tanzania maana anakubalika hata na wapinzani kwani katika wizara zote alizopita, amefanya kazi kwa uadilifu mkubwa na ndiyo maana anakubalika". Alisema Mtaturu.

Aidha alisema kuwa kutokana na kukubalika huko kwa Dkt.Magufuli, kumepelekea Viongozi wa upinzani hususani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kushindwa kumtangaza mgombea urais wao na badala yake wanazunguka kuhubiri Ukabila wakisema wakisema kuwa si Msukuma wakati Watanzania hawamchagui rais kwa kabila lake.

"Wamekosa ajenda na sasa wanasingizia ukabila na kusema kuwa Magufuli si Msukuma, sasa mimi nasema kwa kuwa wamekosa ajenda watashindwa tu katika uchaguzi wa mwaka huu". Aliongeza Mtaturu.

Mtaturu alibainisha kuwa Mchakato wa Kuwapata wagombea wa nafasi za Udiwani na Ubunge ndani ya CCM unaendelea vyema na kwamba chama hicho kitahakikisha kuwa kinawasimamisha wagombea wanaokubalika na wananchi, lengo likwa ni kuibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa mwaka huu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akihutubia katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akihutubia katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza.
Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda akisalimia katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza.
Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda akitia neno katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza Isaack Kalleiya (Kushoto) alipata nafasi ya kusalimia katika Mkutano huo ambapo aliwasihi vijana kutokubali kutumika kisiasa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba wanakiunga mkono Chama cha Mapinduzi CCM katika Uchaguzi wa Mwaka huu. Kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Acheni Mwinshehe (Kulia) akisalimia katika Mkutano wa CCM uliofanyika jana katika viwanja vya Mirongo Jijini Mwanza. Kushoto ni mwenyeji wake Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda.
Viongozi na Makada wa CCM Mkoa wa Mwanza wakifuatilia Mkutano wa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza jana.
Mtia nia Kata ya Mbugani (CCM) Hussein Athuman Kimu (Katikati) pamoja na makada wengine wakifuatilia Mkutano wa CCM uliofanyika jana katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza. 
Kimu anasema "Mabadiliko ni leo na sasa, Chagua Diwani Hussein Kimu, Mtetezi wa Wanyonge Kata ya Mbugani".
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Mirongo jana kwa ajili ya kuwahutubia wananchi.
Waliokaa ni baadhi ya Watia nia ya Kugombea Udiwani Kata ya Mirongo na Mbugani ambapo Kata ya Mirongo kuna watia nia Watano huku Kata ya Mbugani ikiwa na Watia nia 12.
Makada wa CCM na wananchi wa Jiji la Mwanza wakifuatilia Mkutano wa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza jana.
Makada wa CCM na wananchi wa Jiji la Mwanza wakifuatilia Mkutano wa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza jana.
Makada wa CCM na wananchi wa Jiji la Mwanza wakifuatilia Mkutano wa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza jana.

No comments:

Powered by Blogger.