LIVE STREAM ADS

Header Ads

MICHUANO YA KOMBE LA MEYA JIJINI MWANZA KUANZA KURIMBINA WIKENDI HII.

Na:Oscar Mihayo
Michuano ya soka ya kombe la Meya (Meya Cup 2015) Jijini Mwanza, inatarajia kuanza kulindima jumapili Julai 19 katika Uwanja wa Nyegezi Kona  huku yakitarajia kuwa na timu shiriki 24 kutoka katika Wilaya ya Nyamagana. 

Akiogea jana na wanahabari kwenye ukumbi wa Halimashauri ya jiji la mwanza, juu ya uzinduzi wa michuano hiyo ya mwaka 2015,  Mratibu wa mashindano hayo Stanslaus Mabula ambaye ni meya wa jiji la Mwanza anaemaliza muda wake, alisema Lengo la mashindano ni kuwezesha vikundi vya ujasiriamali, kuleta umoja, hamasa, mshikamano na burudani.

“lengo kubwa la mashindano haya ni kuleta hamasa ya michezo kuwezesha vikundi vya ujasilimali kuleta umoja lakini pia kuleta ajira kwa vijana wetu wa jiji letu ikiwa moja ya kuondokana na umasikini na kuwa tegezi kwenye familia”aisema Mabula.

Mabula aliongeza kuwa anaipongeza kampuni ya SBC kupitia kwa kinywaji chao cha Pepsi kwa kuwa mdhamini wa michuano hiyo takribani miaka mitatu ambapo aliiomba kampuni hiyo kuendelea na ufadhiri huo ili kusaidia kuibua zaidi vipaji vya wanasoka.

Aidha mwenyekiti wa michuano hiyo Mohamed Bitegeko alizitaja zawadi kwa mshindi wa kwanza kuwa ni medali ya dhahabu, Bajaji ya magurudumu matatu yenye thamani ya Tsh 6,000,000, na fedha taslimu 2,000,000 na  kombe kubwa, mshindi wa pili ni pikipiki aina ya Tvs yenye thamani ya Tsh 2,000,000 medali ya silver  na fedha taslimu milioni 2,000,000 na mchindi wa tatu atajinyakulia kitita cha Tsh 1,500,000 na medali ya shaba.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa Timu hazitaruhusiwa kusajili wachezaji wanaozidi 25 pamoja na wanaocheza Ligi Kuu ya Vodacom na ile ya Daraja la Kwanza.

Alisema timu itakayomchezesha mchezaji ambaye hayupo kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa itapoteza michezo yote ambayo mchezaji huyo aliichezea kulingana na kananu na sheria za  mashindano hayo.

Bitego alizitaka timu zote kujiandaa vya kutosha ili kuleta hamasa ya mchezo na kuibua vipaji ikiwa na kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa ufunguzi kati ya milongo na Mkolani.

No comments:

Powered by Blogger.