SEHEMU YA NNE: JIFANYIE UCHUNGUZI KATIKA MAMBO YAFUATAYO MAISHANI MWAKO.
HUMPHREY MAKUNDI (KULIA) NA
ALLARD MINJA (KUSHOTO), WOTE WANATOKA LIFE SECRETS COMPANY MWANZA.
4.TISHIO NI NINI
Nipo na kamusi yangu ninayoipenda ya webster
naangalia maana ya tishio(threat) na inasema; Ni mtu au kitu ambacho kinaweza
kuleta shida au madhara.
Sasa usichanganye maneno haya mawili
tishio(threats) na vizuizi(restrictions) maana vizuizi ni kitu kingine kabisa
ambacho kinamaanisha sheria au utawala ambao unazuia au kuthibiti kitu.
Katika maisha yetu ya kila siku kuna baadhi ya
vitu ambavyo tukiwa na tabia ya kuvifanya huwa vinazuia uwezekano wa kupata
kile ambacho tunakihitaji kukipata kwa kiasi kikubwa na hivi vitu ndivyo
vinaitwa tishio au kiingereza threats.
Tishio katika maisha yako wewe ni nini, je ni
pombe ambazo umekuwa unakunywa kila kukicha na ukajikuta unakojoa mabati,
mifuko ya theluji na misumari kila siku? au labda wewe mzuri sana katika
kupoteza muda kwa mambo yasio na maana, au labda wewe ni bingwa wa kuvuta
sigara na unajifanya huoni lile onyo la uvutaji sigara ni hatari kwa afya yako
au pengine wewe ni bigwa wa kuvuna vitu ambavyo haujavipanda(mwizi), tambua
siku wakikushika watakuchoma moto.
Mimi tishio katika maisha yangu lilikuwa
kuangalia movie na siries, nafurahi sana siku hizi sijui siries au muvi ni nini
na nilikuwa nikipoteza muda mwingi sana kwenye kuangalia hivi vitu ambavyo
kimsingi sijawahi kuona faida yake kwangu ukilinganisha na muda niliokuwa
napoteza kuangalia.
Kuna kitu kinaitwa utumwa, unajua mtu kuwa
mtumwa sio mpaka avalishwe sare na afungwe gerezani. Unaweza ukawa mtumwa ukiwa
huru, mfano kama wewe unapoteza zaidi ya masaa mawili kila siku kuangalia box
lenye pembe nne (Tv)wewe ni mtumwa na unatakiwa kutafuta namna ya kujikomboa
kutoka katika utumwa huo.
Hebu fanya hesabu rahisi kabisa kwa watu 100
wanaopoteza muda wa masaa masaa kuangalia lile box (Tv, Movie,series) tena kwa
vitu visivyowajenga kila siku, kumbuka wanafanya hivi muda ambao miili yao bado
ina nguvu na ingeweza kufanya kazi lakini wanaamua tu kuangalia lile box na
kupoteza muda.
Angalia watu 100 wanaopoteza muda pasipo
sababu za msingi, Ngoja nichukue kikokotoleo changu, niweze kupiga mahesabu kwa
watu 100 Tu ambao wanapoteza muda wa saa nne kuangalia Tv hawafanyi kazi yoyote
ya msingi na ni vijana wenye nguvu na afya tele.
Ngoja nikuonyeshe wanarudisha taifa nyuma kiasi gani,
100x4=400 watu 100 wanapoteza kila siku masaa 400 hii ikiwa inamaanisha
kama wangefanya kazi, taifa lingepata masaa 400 ya ziada ila wanayapoteza
maadamu wanaangalia box.
Nagawanya hapa kwa 24 ili nipate siku, 400/24=16.66 tufanye siku 16
Kwa hivyo hawa watu 100 wanaoangalia Tv masaa
4 kila siku wanarudisha taifa nusu mwezi kila siku maana hawafanyi kazi
ipasavyo.
Sasa fikiria watu 1000 inakuwa vipi je watu
10,000 je watu 100,000 ambao hawafanyi kazi wanaangalia Tv tu, taifa linarudi
nyuma kiasi gani.
Kwa hesabu la haraka kama ningeendelea na kikokotoleo changu
ina maana kama watu 100 wanapoteza nusu mwezi kila siku kwa kuangalia tv masaa manne, Ina maana kwa mwaka wangepoteza miezi 6 hivyo watu hawa 100
wanaopoteza muda wanarudisha taifa nyuma miezi sita kila mwaka.
Sasa piga mahesabu ya watu 1000, 10000, 100000, Milioni na
kadhalika uone balaa lake. Eeeeeeh ndio nakuonesha
namna unavyopoteza muda ni lazima utumie muda wako vizuri mafanikio yamefichwa
katika muda kila mtu ana masaa 24 tofauti ipo kwenye namna gani unatumia mda
wako.
Hebu tuangalie tishio lingine la madawa ya
kulevya. Mtakuwa mashahidi wazuri kwamba wanamuziki wengi na vijana wa
hapa nchini kwetu wamekuwa wakipatwa na tishio moja kubwa ambalo ni kutumia
dawa za kulevya kitendo, hiki kimekuwa kikisababisha madhara katika afya zao, miili
yao,familia zao,jamaa na rafiki zao na nchi kwa ujumla maana nchi yetu imekubwa
na kashfa mbaya,na hii inachafua sifa ya nchi yetu.
Hebu kaa chini tafakari ni watu wangapi leo
hii wamepoteza maisha yao kwa kutumia dawa za kulevya?
Na je ni mzigo mkubwa kiasi gani wamekuwa
wakitwika familia zao ? haya ni maswali magumu kuyameza na tunahitaji Kumwomba
Mungu atuokoe katika hili janga na kwa kiasi kikubwa vijana ndio wamekuwa wakiathirika
na haya madawa, hii ni hatari maana vijana ndio nguvu kazi ya taifa.
Tofauti kubwa kati ya vijana na wazee ni
kwamba vijana wanaweza wakatumia akili pamoja na nguvu kwa wakati mmoja lakini
wazee ni akili tu nguvu hawana.
Hebu jifunze namna ya kuepukana na hilo Tishio
ambalo ndio linasababisha wewe kutokuendelea katika maisha yako, kumbuka kila
kitu kinaweza kikabadilika kama kweli ukiamua kujifunza na ukanuia kwamba
unataka madadiliko.
Vijana wenzangu tuamke na tufanye kazi kwa
akili na nguvu zetu, achana na mambo ya vijiweni, piga kazi na jifunze kila
siku, tembea na waliofanikiwa na lazima nawe utafanikiwa.
Itaendelea...
IMEANDALIWA NA LIFE
SECRETS COMPANY YA JIJINI MWANZA AMBAO NI WATAALAMU WA AFYA NA MAENDELEO
BINAFSI.
Email:
allnhumph@gmail.com Phone: 0689 45 26 70/0765 53 68 42
Soma HAPA Sehemu ya Tatu
No comments: