LIVE STREAM ADS

Header Ads

HATIMAE MWANAMUZIKI JULIANA PATRICK AACHIA VIDEO YA WIMBO WAKE UITWAO DEAR DIARY.

Msanii Juliana Patrick
Na:Binagi Media Group
Hatimae yule mwanamuziki Juliana Patrick ambae ni binti wa Kitanzania anayeishi Jijini Houston Texas nchini Marekani kwa ajili ya Masomo yake, ameachia video yake ya kwanza ya kibao chake kiitwacho "Dear Diary".

Video hiyo iliachiwa rasmi katika siku yake ya kuzaliwa ambayo ilikuwa ni jumapili ya July 12 mwaka huu jijini humo.


Binti huyu ambaye ametimiza miaka 16 sasa, tayari ameshaachia ngoma tatu ambazo zimepokelwa vyema. Ngoma hivyo ni Dear Diary (ambayo video yake imetoka), Remember Me pamoja na We Are On A Roll. 

Jambo jema zaidi ni kwamba nyimbo za Juliana Patrick ambae ni binti wa Kisukuma 
kutoka Isolo Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza ni kwamba zimepokelewa vizuri pia hapa nchini Tanzania. 

"Dear Diary is being played on Tanzanian radios!! Asanteni sana!! #DearDiary This is just the beginning". Juliana Patrick aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitta akizishukuru radio za Tanzania kwa kuucheza Wimbo wake wa Diar Diary na kusema huo ni mwanzo tu.

Kubwa zaidi Kibao cha Dear Diary kilipotoka tu mwishoni mwa mwaka jana kilipanda chati na kufikia Nambari mbili katika chati za muziki huko Texas nchini Marekani.

Hakika ni wakati wako ewe Mtanzania kuungana na Juliana Patrick katika kuzidi kuufanya muziki wake usonge mbele zaidi ili nyota yake ya Muziki ipate kupamba moto na hatimae kuipeperusha Vyema Bendera ya Tanzania katika anga la muziki Kimataifa.


Bonyeza HAPA Kusoma zaidi au Bonyeza HAPA Kupata nyimbo zote za Juliana Patrick.

Search Juliana Patrick Youtube ili kutazama Dear Diary au Bonyeza Play hapa chini.

No comments:

Powered by Blogger.