WAFANYABIASHARA 20 WATIWA NGUVUNI KWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA UVUNAJI WA MISITU BILA KIBALI.
Takribani Wafanyabiashara 20 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani
katika kipindi cha mwaka 2014/2015 kutokana na kujihusisha na uvunaji holera
pamoja na usafirishaji wa mazao ya
misitu kinyume cha sheria.
Hayo
yalibainishwa jana na kaimu Meneja wa Wakala wa Misitu Kanda ya ziwa, Ngatara
Kimaro alipokuwa akizungumza na Radio Metro kuhusu hali ya misitu katika Ukanda
wa ziwa.
Alisema
kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika beria za Kamanga, Jijini
Mwanza, Biharamulo Mkoani Kagera, Busisi na Usagara Wilayani Misungwi.
Alibainisha kuwa hali ya misitu katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ni kwa ujumla kutokana
na watu kutofuata utaratibu wa uvunaji wa mazao ya misitu na hivyo kuvuna mazao
hayo kihorera jambo ambalo linaweza kupelekea kuwepo kwa majanga mbalimbali
ikiwemo ukosefu wa mvua za kutosha.
Kimaro alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili ofisi ya Wakala wa Misitu
Kanda ya Ziwa kuwa ni pamoja na ushirikiano duni na wananchi katika kulinda
misitu, uchache wa watumishi pamoja na uchache wa vitendea kazi ambapo ameiomba
serikali kuzishughulikia changamoto hizo ikiwemo kuongezea ulinzi kwa ajili ya
kuendelea kupambana na waharibifu wa misitu.
No comments: