LIVE STREAM ADS

Header Ads

SEHEMU YA TATU: JIFANYIE UCHUNGUZI KATIKA MAMBO YAFUATAYO MAISHANI MWAKO.

3.FURSA
Hii nafasi au hali ambayo inaleta uwezekano wa kufanya kitu ambacho unataka kukifanya, ni uwezekano wa kufanya kitu fulani.
Kuna siku niliwahi kuandika kwamba kama hauna mpango kwenye maisha yako hata kama zipo fursa mahali unapoishi hauwezi kuziona. Huu ni ukweli usiokuwa na upinzani wa aina yoyote.

Tunajua fika kwamba binadamu anaona kupitia macho lakini ukweli ni kwamba haoni kwa macho bali anaona kwa ubongo na kama ulikuwa hujui hili soma basi fahamu tu kwamba macho ni kiungo cha fahamu kinachokusaidia kutazama vitu vilivyopo nje lakini huoni kwa macho unaona kwa ubongo.

Mtu anapokuwa na mpango kwenye maisha yake kama kwenye jamii yake kuna fursa basi ni dhahiri kwamba ataziona maadamu tayari ana mpango fulani na ubongo wake ndio utakaomuonesha kwamba katika tatizo hili ambalo wanajamii wanajilaumu na hawapati suluisho wewe unaweza kulitatua kwa kutumia kipengele fulani katika ule mpango anaokuwa nao.

Ukikosa mpango katika maisha yako hapo unakubali vitu vilivyoko nje vitawale vilivyoko ndani jambo ambalo sio sahihi kabisa kinachotoka ndani ndicho kinatakiwa kitawale kilichopo nje. 

Unajua usikubali maisha yakupangie wewe unatakiwa kuwa na nini, na nini hautakiwi kuwa nacho,wewe ndio unatakiwa kuyapangia maisha na kuyatawala, usikubali kutawaliwa na maisha kama watu wengi wanavyotawaliwa nayo maana kuna watu ni mabingwa wa kupokea chochote maisha yanachowapa na ubaya ni kwamba hayatakupa zaidi ya njaa, umaskini, mahangaiko, masononeko, ushirikina n.k

Tunaishi duniani kwa muda mfupi hivyo tujitahidi basi kuona fursa na kuzitumia ili uishi kwa furaha maana fursa hawajaumbiwa watu fulani tuu bali ni kwa kila mtu na wewe ni mmoja wao.

Jifunze basi namna ya kupanda miti,jifunze namna ya kutengeneza vitu mbalimbali,jifunze vitu vingi kadiri ya uwezo wako kisha vitendee kazi katika maisha yako. Sasa wewe unasema hakuna fursa alafu unakaa nyumbani? Hivi unajua njia ya kuushinda woga ni kutoka hiyo sehemu ulipo na kufanya kitu? Sasa basi uache kulalamika kwamba hakuna fursa, unajua kiuhalisia nimekuja kugundua kwamba kazi zipo ila kwa kiasi kikubwa huwezi kusikia zikitangazwa. 

Angalia mfano huu Less Brown wakati anahangaika kuanza maisha yake alikuwa anapenda kuwa mtangazaji, mara kadhaa alienda kuomba kazi kwenye radio moja hivi lakini alikuwa akiambiwa hakuna kazi na bosi kumfukuza kwa kumtuhumu ni king'ang'anizi.

Siku ya kwanza alienda akaambiwa hakuna kazi watu wamejaa kila idara, siku ya pili akaenda bosi akamkaripia akamwambia si jana tu nimekuambia hakuna kazi, akamwambia alidhani kuna mtu kaacha kazi kwa hiyo kaja kuchukua nafasi yake, bosi akamfukuza na kumwambia hakuna alieacha kazi, mara ya tatu kaenda tena na kudai kwamba alidhani mtu kafa siku iliyopita, mara ya nne akaenda akasema simu yake ilipotea akahisi huenda bosi alimpigia simu asimpate, kadhalika na ya tano akaenda na sababu, siku ya sita alipofika ofisini bosi alipomuona akacheka akamwambia nenda kanichukulie kahawa na kazi akapata. 

Kwa nini nimekuandikia hii stori, ni kukuonesha kwamba fursa zinakuwepo sema hutakiwi kukata tamaa mapema pindi unapozihangaikia hizo fursa na saa zingine watu huwa wanapima tuu uvumilivu wako.

Asikudanganye mtu fursa zipo nyingi sana hivyo ni suala la kufikiri na kuwa na mtazamo sahihi tu ndilo linatakiwa ili uweze kuziona hizo fursa sema ubaya wa asilimia 90 watu wanaona kwa macho siyo akili kwa hiyo wanakuwa hawawezi kuziona hizo fursa.

Nawiwa kukuambia namna gani mtu anafikiri, mtu huwa anafikiri kwa picha na kama hakuna picha mtu huchanganyikiwa au anaweza asikuelewe, nikisema gari lako, kinachokuja kwenye akili yako ni picha ya gari, je nikisema friji,je mke wako,je mme wako,je mtoto wako,Je rais wa awamu ya nne Tanzania,je nikisema Barack Obama umeona eeeh kinachokuja ni picha ya hivyo vitu ndio maana ukiwa unamuahadithia mtu kitu ili akielewe vizuri inakubidi umuhadithie kiufasaha mpaka apate picha halisi ya hicho kitu maana tunafikiri kwa picha.

Tengeneza picha halisi ya kitu unachokitaka kwenye akili yako na hakikisha unakiona kikoje kisha anza kufanya jitihada zote za hicho kitu ambacho umetengeneza picha yake na usifanye kitu ambacho hujatengeneza picha yake katika akili yako, kama unataka kuwa rubani basi anza kujiona mapema kabisa unaendesha ndege, mkandarasi anza kuona namna unavyofanya kazi ya ukandarasi na watu wanasifia kile unachokitenda kuwa ni kizuri,mwanahabari anza kujiona unaripoti habari kadha wa kadha kwa ufasaha na una mafanikio katika kile unachokitenda, fanya kama wanavyofanya Salumu Kikeke, Charles Hillary, Maulid wa Kitenge, Millard Ayo, George Binagi, Alphonce Tonny Kapela na wengineo wengi wanaofanya vizuri katika tasnia uipendayo na hapo utaona mafanikio yake.
Itaendelea...
IMEANDALIWA NA LIFE SECRETS COMPANY YA JIJINI MWANZA AMBAO NI WATAALAMU WA AFYA NA MAENDELEO BINAFSI.
Email: allnhumph@gmail.com Phone: 0689452670/0765536842
Soma HAPA Sehemu ya Pili

No comments:

Powered by Blogger.