LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKALA "MAFANIKIO SIYO AJALI" SEHEMU YA PILI.

Soma HAPA Sehemu ya Kwanza ili Twende Sote
Unajua watu wengi hawajawahi kujiuliza maswali kama haya hapa... Kwa nini Mungu aliumba mito? Kwa nini Mungu aliumba Miti? Kwa nini Mungu aliumba chuma? Mungu hakukupa vitu vilivyotimia kwa sababu anajua una asili ya uumbaji ndani yako maana umeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, hivyo basi hakukupa vitu vilivyokamilika ila alikupa vitu ambavyo vitakupelekea kutengeneza vitu vingine ili uendeleze ule uumbaji ambao yeye aliuanzisha ,tunajua kabisa kwamba Mungu ni asili ya uumbaji.
Nataka nikwambie hivi binadamu kawekewa uwezo wa ajabu sana ndani yake na Mwenyezi Mungu wa kutenda mambo makubwa na ya ajabu ndio maana Mungu hakukupa vitu vilivyokamilika kama magari, nyumba, ndege,umeme,meza, n.k ili aliweka ndani yako uwezo wa kutumia mito ukaweka madaraja juu yake na magari yakapiti lakini pia alijua kabisa unao uwezo wa kutumia mito ukatengeneza mitumbwi ikapita, lakini pia alijua unao uwezo wa kutumia maji ukatengeneza umeme na ukautumia huo umeme kwa matumizi mbalimbali kama kwenye viwandani,manyumbani,maofisini na kadhalika.
Pia Mungu aliumba miti hakuumba meza, wala vitanda ,wala viti,wala mkaa kwa sababu anajua unao uwezo wa kubadili hivi vitu kuwa vitu vingine kwa ajili ya matumizi yako na pia ukaendeleza uumbaji wake.
Hebu angalia tena fikiri kwa kina Mungu kaumba chuma lakini hakuumba gari ila ndani yako wewe kama mwanadamu aliweka uwezo wa kutengeneza magari kwa kupitia zile chuma. Sasa swali nakuuliza katika vitu vyoote Mungu alivyotupa bure kabisa kuna ardhi,kuna maji, kuna anga,kuna hewa, kuna bahari, kuna maziwa na vingine vingi wewe umetumia kipi kuendeleza uumbaji wa Mungu hii ni changamoto kwangu na kwako.
Hebu tazama wright Brothers waliweza kutumia anga kutengeneza ndege, Hivi unajua kwamba katika kikao cha mwisho kilichojumuisha wanasayansi 64 wote walisema kwamba haiwezekani kutengeneza ndege ikapaa hewani? Na je unajua kwamba hao wenyewe tuu ndio walibakia katika kikao kile wakisema kwamba inawezekana? Na je unajua Baba yao aliwaambia wakifa watachomwa moto kwa kuwa na mawazo kwamba inawezekana kutengeneza ndege na kuirusha angani? Leo ndege zipo au hazipo?
Nafurahi hawakumsikiliza yeyote walisimamia wazo lao waliamini inawezekana na kweli mwisho wa siku waliweza Leo hii tunasafiri kwenda sehemu mbalimbali duniani pasipo shida ya aina yoyote kwa sababu ya wright Brothers, ushawahi kujiuliza kama kungekuwa hakuna ndege tukawa tunasafiri na mabasi au meli ingekuchukua mda gani kutoka hapa Tanzania kufika Marekani au Brazil au Canada au Wingereza? Bila shaka ungesafiri hata miezi miwili mitatu na bado usingefika. Mungu awapumzishe pepa peponi asante Mungu kwa kuwaumba,
Nakuja kwako wewe je una mipango mingapi umeiacha kisa watu wamekuambia haiwezekani? usiwasikilize nakwambia maana watu wengi wameshindwa kutimiliza ndoto zao kwa kusikiliza watu hata kama ni mzazi wako, hata kama ni rafiki,hata kama ni ndugu ivi kweli jaribu kutafakari haya maneno kwa kina kama tungefanya kama wazazi wetu walivyofanya mabadiliko yangekaa yatokee? wright brothers wangemsikiliza baba yao leo tungekuwa na ndege?anza kushughulikia mpango wako maadamu unauona katika fikra zako ina maana unaweza kuutimiliza mimi nakuhakikishia hakuna kitu kitakachoweza kukuzuia kupata kile unachokitaka labda tuu uamue kujizuia mwenyewe ila kama kweli umenuia kukitafuta kwa moyo wako wote na ukafuata taratibu zote za kukitafuta utakipata tuu na sina wasiwasi katika kusema hivi.
Naomba nimalizie kwa kusema hivi kitu pekee kitakachokuzuia kupata kile unachokitaka ni wewe mwenyewe na kingine ni kuruhusu mawazo ya watu wengine kutawala mawazo yako kwamba huwezi ukafanikiwa katika hilo unalotaka kufanya.
Tuendelee kesho...
Imeandaliwa na; Life Secrets Company 
PHONE:0689 452/670 /0765 536 842 EMAIL: allnhumph@ gmail.com

No comments:

Powered by Blogger.