LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKALA: MATATIZO NI NGUZO YA MAFANIKIO.

Mtu ambae hafikiri vizuri anadhani kwamba maisha hapa duniani yangekuwa mazuri kama kungekuwa hakuna matatizo. Biashara ya mafanikio sio kufanikiwa tuu bali ni kujua namna ya kutatua matatizo ambayo yanakuwa yanamkumba mtu katika maisha kwa kipindi fulani.
Lakini matatizo ndio yanafanya maisha kuimarika na kuwa mazuri kila iwapo leo..Kitu ambacho watu huwa hawajui ni kwamba watu waliofanikiwa ni wale waliojifunza namna ya kutatua matatizo mbalimbali katika jamii yao pamoja na maisha yao kiujumla, huwezi kufanikiwa kama hujui namna ya kutatua matatizo mbalimbali yanayojitokeza kwenye jamii yako.
Ifahamike kwamba kadiri mtu unavyokuwa na matatizo na kuweka kikomo cha kutatua matatizo ya mambo fulani yanayomkabili ndio kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kufanikiwa maana akili ya binadamu inafanya kazi zaidi pindi anapokuwa kwenye matatizo na anafanya kila jitihada za kujitahidi kutatua lile tatizo ambalo linakuwa linamsumbua.
Kitu kinachonishangaza hapa nchini kwetu ni kwamba watu wengi wana matatizo lakini bado hawataki kujifunza vya kutosha namna ya kutatua matatizo mbalimbali ambayo yanawakabili na hali hii imekuwa inawafanya wasiwe na mabadiliko kutoka mwaka mmoja mpaka mwaka mwingine, ukimuacha mwaka huu ukija baada ya miaka miwili yupo vile vile kimaendeleo cha zaidi atabadilika mwili tuu.
Wengi hawajui kwamba moja ya tajiri mkubwa hapa Tanzania alipata wazo la biashara baada ya sehemu ambayo aliyokuwa anaishi kuwa na tatizo la peni kipindi hicho zilikuwa zinaitwa bic basi baada ya kumshirikisha mke wake akamwambia kwa nini usianze kufanya biashara ya kuuza hizo kalamu maana hazipatikani hapa nchini kwetu? 
Kama kawaida ule msemo wa watu wengi sina mtaji ukatawala maongezi yake lakini baada ya muda aliamua kwamba atafanya hiyo biashara kwa mali kauli,basi akaanza hii biashara akaenda Kenya akawa anazisafirisha bic zake anakuja kuuza hapa nchini leo hii huyu Dr. ana utajiri wa zaidi ya dola za Kimarekani millioni 550. Unataka kumjua ni nani? Ni Dr. Regnald Mengi mmiliki wa kampuni ya IPP media group.
Ukitaka kuamini nguvu ya akili yako katika kutatua matatizo hebu kajaribu kufanya jaribio hili nimejifunza kwa Pastor mmoja mashuhuri aliekuwa anaitwa Dr. Norman Vincent Peale fanya hivi....nenda katafute mtu mwenye matatizo zaidi yako kisha msaidie kutatua matatizo yanayomkabidili baada ya hapo uone nguvu na namna utakavyojiamini baada ya kumsaidia kutatua tatizo lake.
Wote huwa tunakuwa kwenye matatizo kwa wakati fulani lakini baada ya kujiuliza ni jambo gani tunaweza kulitenda ili kutatua tatizo ambalo linatusumbua ndipo tunafikiri zaidi wazungu wanasema to think outside the box yaani kufikiri nje ya box tufanye kazi kwa kujituma tukiamini kwa kufanya ivo hali yetu itabadilika na maisha kuwa mazuri zaidi ,tubuni na tuje na mbinu mpya za kufanya mambo mbalimbali na mwishowe tutafanikiwa katika maisha yetu.
Tatizo la giza ndilo lilimfanya Edison akatengeneza balbu na kugundua namna 9000 ambazo balbu ya umeme isingeweza kufanya kazi,tatizo la kutokuona vizuri ndilo lilifanya watu wakagundua miwani ambayo ina lenzi ya kumwezesha mtu asieona vizuri kupata kuona tena, tatizo la kutoa harufu mbaya ndio lilimfanya mtu akagundua dawa ya meno leo hii unanunua unaitumia kila siku na matatizo mengineyo ambayo watu wamekuja na namna mbalimbali za kuyatatua.
Nataka nikupe wazo la kuanza biashara leo bure kabisa hebu kaa chini chukua peni na karatasi kisha andika ni vitu gani unaona haviko sawa katika jamii yako na baada ya kuviorodhesha anza kuvitendea kazi..tayari wazo la biashara ushapata kama ulikuwa hauna, anza kulipangilia namna utakavyolifanya, anza kufikiri utamshirikisha nani kisha anza kulifanya mara moja kabla watu wengine hawajakuwahi.
Hebu tujifunze kuona matatizo kama fursa jua hivi nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ndipo kuna fursa nyingi za kuweza kukufanya wewe kufanikiwa maana matatizo yanapokuwa mengi ndipo uwezekano wa wewe kufanikiwa unakuwa mkubwa sana.
Mwisho
KUANZIA TAREHE 14/09/2015 AWAMU YA PILI YA KUJIFUNZA KWA AUDIO NA MAANDISHI HAPA HAPA WHATSUP ITAANZA TENA ZIPO MADA ZAIDI YA 15 JIANDIKISHE MAPEMA MSHIRIKISHE NA RAFIKI YAKO.
WASILIANA NASI WHATS KWA 0689452 670 KUJIANDIKISHA TUMIA WHATSUP KUONGEZA MAARIFA. WANAOTAKA KUANDIKA BUSINESS PROPOSALS, BUSINESS PLAN, FUNDS PROPOSALS NA ANDIKO LOLOTE WAPASHE HABARI HII PIA.
KUMBUKA MAKALA ZETU UNAWEZA KUZISOMA BINAGI MEDIA BLOG, MJUMBE BLOG NA BAADHI KWENYE GAZETI LA MWANACHI.
TUNAKUTAKIA SIKU NJEMA, SHEA NA RAFIKI ZAKO WENGI KADIRI UWEZAVYO, SIKU NJEMA , LIFE SECRETS COMPANY!

No comments:

Powered by Blogger.