LIVE STREAM ADS

Header Ads

SEHEMU YA PILI YA MAKALA IITWAYO "NIA".

Soma HAPA Sehemu ya Kwanza
Wakati umetambulishwa kwa mtu mwingine unayo nafasi ya kipekee ya kujiuza mwenyewe kwa huyo mtu kwa kiasi cha NIA utakachokionesha wakati unatambulishwa, wakati unasalimiana kwa kushikana mikono na mtu mwingine unayo nafasi ya kipekee ya kumvutia yule unaesalimiana nae kwa kuongea maneno yenye NIA ambayo utayaambatanisha wakati mnasalimiana kwa kushikana mikono, watu hawapendi watu wanaosalimiana na mikono iliyolegea salimia kijasiri washa NIA utajiuza vya kutosha kwa unaesalimiana nae.
WAKATI UMEKUTANA NA MTU MWINGINE.
Washa NIA yako na hakikisha unatumia maneno mazuri na sauti nzuri yenye ujasiri kiasi ambacho kitamfanya huyo mtu unaewasiliana nae ajisikie furaha kuwasiliana na wewe. Acha kusalimiana na watu huku umekunja sura au unatoa sauti ya manung'uniko hii itamfanya yule mtu unaesalimiana nae asitake hata kusikiliza unachotaka kumwambia.
Wakati mnasalimiana kwa kushikana mikono fanya hivyo kwa ukakamavu na katika kila mwisho wa maneno yako sema haya maneno Ninafurahi sana kukutana na wewe. Hii pia ni muhimu sana kwa watu wanaofanya biashara ya mtandao.Usimfuate mtu kizembe kizembe, nenda kwa ujasiri na salimiana nae kwa kujiamini na hakikisha unamwangalia usoni pindi unapoongea nae na hii itazidi kumvuta karibu na wewe lakini pia atakuona unajiamini na unaamini hicho unachotaka kumuuzia ni sahihi kwake.
Wakati umeanza kuwasiliana hakikisha kwamba unapeleka mawasiliano yako kwa huyo unaewasiliana nae kiasi ambacho atajisikia vizuri kwa muda ule, acha kuwasiliana na mtu huku unafanya mambo mawili kwa wakati mmoja, kwa mfano unaongea na mtu ambaye ni kwa mara ya kwanza kukutana nae huku unaandika meseji kwenye simu, hapo yeye atatafsiri kama umemdharau lakini pia akili ya binadamu ambayo haijalala haiwezi kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja( conscious mind). 
Acha kujidai unajua kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja (multitasking) kuna sehemu zingine multitasking huponza na kuharibu kila kitu.
Mfuatilie kwa umakini mtu yule unaewasiliana nae kama kuna mahali hujamuelewa hakikisha unamuuliza swali hii pia itamfanya uwepo wake uwe nawe wakati unajaribu kujiuza kwake(selling yourself) kwa kufanya na kutumia hizi mbinu basi huyo mtu uliekuwa unaeongea nae kuhusu maslahi yako, au biashara zako,au wazo lako fulani atakuwa amekusikiliza kwa umakini na kwa kiasi kikubwa utakuwa umeuteka uwepo wake hivyo itakuwa rahisi wewe kumuuzia huduma fulani unayotaka kumuuzia.
Siku moja daktari mmoja alihojiwa ambapo alibainisha kwamba NIA anayoingia nayo wakati anaenda kufanya upasuaji ni moja ya kigezo kikubwa ambacho husababisha mgonjwa anaemtibu kupona katika ule upasuaji. Kama angeingia bila NIA ya kutosha ni dhahiri kwamba mgonjwa wake hawezi au utasikia ameacha mkasi ndani mwili wake baada ya upasuaji na pengine upasuaji kwake unaweza usifanyike vizuri.
Umeona NIA ni katika kila jambo ambalo unalifanya hivyo ili ufanikiwe ni lazima uweke NIA. Usipoweka NIA sahau kufanikiwa watu wanaofahamu faida za kuwasha na kuzima NIA zao ukiwafuata watakuambia.
Itaendelea...
IMEANDALIWA NA LIFE SECRETS COMPANY.

No comments:

Powered by Blogger.