ASKOFU GWAJIMA ASEMA DKT.SLAA NI MUONGO. AKANUSHA MAASKOFU KUNUNULIWA NA MHE.LOWASA.
Na:Binagi Media Group
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Josephat
Gwajima (Pichani) amekanusha tuhuma zilizotelewa juu yake pamoja na Maasikofu 30 wa
Kanisa Katoliki nchini kuwa wamenunuliwa na Mgombea Urais wa Chama cha
Demokrasia na Chadema anaeungwa Mkono na Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
Ukawa.
Hii ni siku chache baada ya aliekuwa Katibu Mkuu
wa Chadema Dkt.Wilbroad Slaa kutoa shutuma hizo alipokuwa akitangaza kuachana
na siasa kutokana na kutokubaliana na maamuzi ya chama chake ya kumteua
Mh.Lowasa kuwa mgombea urais wake.
Akizungumza hii leo na Waandishi wa Habari
Jijini Dar es salaam, Askofu Gwajima amesema kuwa Dkt.Slaa ni muongo na kwamba
hakuna ukweli wowote dhidi ya tuhuma anazozitoa kwa maaskofu nchini.
“Dkt.Slaa ni muongo, Mababa askofu wa kanisa
katoliki hawakupewa rushwa wala mimi sijapewa rushwa. Kusema amehama Chadema
kwa Ufisadi wa Lowasa ni uongo kwani Mkewe (Josephine Mshumbuzi) ndie aliemzuia
maana alikuwa ameisha anza kuwaambia watu kuwa yeye ndiye First Lady”.Amesema Askofu
Gwajima.
Katika hatua nyingine Askofu Gwajima amesema
kuwa Dkt.Slaa anatumika na kuwataka wanaomtumia kuacha mara moja maana anawaharibia
baadhi ya wagombea huku pia akitoa lawama zake kwa maafisa wa usalama wa taifa.
“Usalama wa taifa sio wa CCM, mnatafasiriwa nyie
ndio mnatukana maaskofu, usalama wa taifa mnamuharibia Magufuli, mwacheni aendelee
na kampeni zake kwa amani. Siku nitakayorudi kumjibu Slaa akinisemesha,
nitasema Slaa alivyokutana na watu wa usalama wa taifa Afrika kusini. Usalama
mtapomuongoza tena huyo mtu wenu wenu atukane maaskofu, nitawalipua na bomu na
macho yenu hamtafungua tena”.Amesema Askofu Gwajima.
No comments: