MATATA AAHIDI KUTOWAANGUSHA WAPIGA KURA WAKE.
Na:George GB Pazzo
Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Kitangiri Wilaya ya
Ilemela Mkoani Mwanza kimezindua kampeni
zake za Uchaguzi ambapo Mgombea Udiwani katika Kata hiyo Henry Mtinda Matata ameahidi
kutekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo endapo akichaguliwa kuwa diwani
katika Uchaguzi wa mwaka huu.
Akihutubia katika Mkutano wa uzinduzi wa kampeni
hizo uliofanyika juzi katika Uwanja wa Minazi Mitatu uliopo Kona ya Bwiru, Matata
alisema kuwa akichaguliwa kuwa diwani wa Kitangiri atahakikisha anaondoa kero
ya maji katika mitaa ya milimani ikiwemo Mitaa ya Ibanda na Mwinuko pamoja na
kufikisha huduma ya umeme katika Mitaa hiyo.
Matata ameongeza kuwa atahakikisha anasimamia vyema
ukarabati wa barabara za Kata hiyo kwa Kiwango cha lami, kuboresha huduma za
afya, kuwawezesha akina mama na vijana kupitia mikopo yenye riba nafuu pamoja
na kutetea haki na maslai ya wazee.
"Mimi nawaahidi kuwa sitawaangusha na nitasimamia vyema
ukarabati wa barabara kwa Kiwango cha lami, nitaboresha huduma za
afya katika zahanati yetu, akina mama watapata mikopo yenye riba nafuu, vijana pia sitawahau, lakini pia nitatetea haki na maslai ya wazee". Alisema Matata.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya
Ilemela ambae pia ni mgombea udiwani Kata ya Igoma Jijini Mwanza Mussa Magabe alisema kuwa ilani ya chama hicho ya mwaka 2015/20 inatoa
fursa ya kimaendeleo kwa makundi yote nchini hivyo Wananchi wasisite kuwachagua
viongozi wanaotokana na Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
Octoba 25 mwaka huu.
TAZAMA PICHA HAPA
No comments: