LIVE STREAM ADS

Header Ads

CCM KUJENGA MABWENI SHULE ZA KATA IKIWA ITAPATA RIDHAA YA KUSHIKA DOLA AWAMU YA TANO.

Judith Ferdinand
Chama cha Mapinduzi CCM kimeahidi kujenga mabweni katika shule zote za Kata nchini ikiwa wananchi watakipatia ridhaa ya kurudi madarakani.

Wito huo ulitolewa juzi na mgombea Mwenza wa urais wa chama hicho Samia Suluhu, katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Kata ya Kisesa wilaya ya Magu mkoani Mkoani Mwanza.

Alisema kuwa akiwa kama mama anatambua  changamoto  wanazo kutana nazo watoto wa kike ikiwemo vishawishi kutoka kwa wanaume  njiani wakati wa kwenda shule na kurudi nyumbani.

Alisema kuwa ili kuwaepusha wasichana na changamoto zinazowakabiri, atasimamia ujenzi wa mabweni kwa ajili ya kuwawekea mazingira bora wanafunzi wa kike.

Alisema ili kuendelea kuwakinga wasichana na mimba pamoja na ndoa za utotoni, serikali ijayo itawapatia wanafunzi elimu bila malipo kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.

"Watoto watasoma shule bila malipo kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne,ili jamii muache kusomesha watoto wa kiume pekee kwa kisingizio cha kutokuwa na fedha za kuwalipia wote, na kuwasababi mimba sambamba na  ndoa za utotoni". Alisema Suluhu.

No comments:

Powered by Blogger.