LIVE STREAM ADS

Header Ads

HIKI NDICHO KILICHOMPA KAYUMBA JUMA USHINDI WA SHINDANO LA BSS 2015.

Mshindi wa Shindano la kusaka Vipaji vya Muziki la Bongo Star Search mwaka 2015 Kayumba Juma ameweza kuibuka mshindi wa shindano hilo mwaka huu ambalo lilikuwa na ushindani mkali kutokana na uimbaji wake wenye kuvuta hisia kali.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Baada ya kazi ndefu ya kuwachuja washiriki wa shindano hilo lililomalizika usiku wa kuamkia leo, washiriki watatu ambao ni Frida Amani, Nasib Fonabo na Kayumba Juma waliingia tatu bora na kufanya majaji kuwa na kazi kubwa ya kufanya.

Hata hivyo alianza kutoka mwanadada Frida Amani na wakabakia washiriki wawili ambao ni Nasib Fonabo pamoja na Kayumba Juma, wote wakiwa wakali.

Hatimae Chief Judge Mada Rita Polsen aliweza kukata mzizi wa fitina baada ya kumtangaza Kayumba Juma kuwa Mshindi wa BSS 2015 ambae amejinyakulia kitita cha shilingi milioni hamsini na ofa kibao ikiwemo kuwa chini ya uangalizi wa kundi za muziki la Tip Top Connection.

Hakika washiriki wote wa BSS 2015 ni wakali hususani waliotinga 10 bora hivyo ni vyema wakaongeza juhudi zaidi na kufikia ndoto zao ikizingatiwa kwamba jukwaa la BSS 2015 walilokuwa litawafungulia milango ya mafanikio zaidi. 
Kayumba Juma akiuchungulia ushindi
Nasib Fonabo aliishia nafasi ya Pili
Frida Amani aliishia nafasi ya Tatu

No comments:

Powered by Blogger.