ESTHER MATIKO (CHADEMA) AIBUKA KIDEDEA JIMBO LA TARIME MJINI.
Na:Waitara Meng'anyi
Aliyekuwa Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Esther Matiko (mwenye kofia) na Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini ameibuka kidedea kwa kura 20017 huku akifuatiwa na Mgombea kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Michael Kembaki aliyepata kura14,025 akifuatia mgombea wa ACT Wazalendo Deogratias Meck aliyepata Kura 356.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi mkuu wa Uchaguzi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Juma Mwajombe amemutangaza Esther Matiko kuwa mshindi katika Jimbo hilo kupitia Chama cha Upinzani huku akifuatiwa mgombe Ubunge kupitia CCM na wa Mwisho ACT Wazalendo.
Akiongea na wandishi wa habari Mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini kupitia upinzani Esther Matiko alisema kuwa wanatarime wategemee maendeleo ya haraka ikiwa ni pamoja na kudai kuwa watanzania wameweza kudhiilishia umma kuwa Mwanamke anaweza kuongoza vyema.
Hata hivyo Matiko aliongeza kuwa kulingana na kura ambazo wamemuchagua wananchi wa Tarime hatoweza kuwaangusha katika suala zima la Maendeleo ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi zote ambazo aliweza kuhaidi katika kipindichote cha kampeni.
Matokeo katika Kata nane za jimbo la mjini yanaonyesha kuwa CCM na Chadema vimetoshana nguvu.
Matokeo katika Kata nane za jimbo la mjini yanaonyesha kuwa CCM na Chadema vimetoshana nguvu.
No comments: