LIVE STREAM ADS

Header Ads

HISIA ZA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA BAADA YA MAGUFULI KUTANGAZWA MSHINDI WA URAIS NCHINI.

Dkt.John Pombe Magufuli (Pichani) ametangazwa kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais katika Uchaguzi uliofanyika jumapili Octoba 25,2015
Na:Binagi Media Group
Msemo wa HapaKaziTu pamoja na push Up za hapa na pale zilitawala kwa asilimia kubwa Jijini Mwanza katika mitaa mbalimbali ya Jiji hilo baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nec kutangaza matokeo ya Urais nchini Tanzania.

Furaha yao iliibuka mara tu baada ya Mwenyekiti wa Nec Jaji Mstaafu Damian Lubuva kumtangaza Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM John Pombe Magufuli kuwa Mshindi wa kiti cha Urais na hivyo kuwa rais wa serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika Mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza ikiwemo Mabatini, Kirumba pamoja na Ofisi ya CCM Mkoa wa Mwanza shamrashamra zilitawala baada ya Dkt.Magufuri kutangazwa kuwa mshindi katika nafasi hiyo ya urais baada ya kupata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 na kufuatiwa na Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kwa mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa Edward Ngoyai Lowasa aliepata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97.

Kwa ushindi huo, Mama Samia Suluh Hassan anakuwa Makamu wa Rais mwanamke wa kwanza nchini Tanzania na hivyo kutoa fursa nyingine mpya ya kiuongozi kwa kundi la wanawake nchini. Wanatarajiwa kukabidhiwa vyeti vya ushindi siku ya kesho katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

Matokeo ya wagombea wengine kutoka Ukumbi wa Kutangazia Matokeo uliopo katika Ukumbi wa Kituo cha Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam ni; Anna Elisha Mghwira, ACT Wazalendo Kura 98,763, Chief Lutalosa Yemba, ADC Kura 66,049, Hashim Rungwe Spunda, CHAUMMA Kura 49,256, Kasambala Janken Malik, NRA Kura 8,198, Lyimo Macmillan Elifatio, TLP Kura 8,198 pamoja na Dovutwa Fahmi Nasoro, UPDP Kura 7,785.

Octoba 29 pia imeingia katika kumbukumbu nzuri za Dkt.Magufuli baada ya kutangazwa kuwa rais mteule wa Tanzania, ikizingatiwa kuwa tarehe na mwezi kama wa leo mwaka 1959 alizaliwa Dkt.Magufuli.

No comments:

Powered by Blogger.